Faraja Saidi na kazi ya Ubunifu

Faraja Saidi na kazi ya Ubunifu

“Mimi ni binti mwenye future ambaye siku moja nategemea kuwa mama, kuwa na familia, natakiwa ni work katika misingi  mizuri ambayo nimelelewa na fashion ndiyo kazi yangu.”

Hayo ni maneno ya Faraja Saidi, mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) akiwa anachukua Degree course ya Marketing and Public Relation, mwaka wa 3.

Akifanya mahojiano na Jarida la Mwananchi Scoop, Faraja ameweka wazi kuwa yeye ni binti mwenye misimamo yake na fashion ndiyo kazi yake licha ya changamoto na dhana mbalimbali, ambapo mara nyingi jamii huwa na mitazamo hasi juu ya kazi hiyo.

Amesema yeye anaithamini kazi hiyo kwa kiasi kikubwa ndiyo maana ikitokea opportunity kuhusu masula hayo huwa anakuwa mwepesi kuitikia.

Vile vile ameeleza fashion ndiyo kazi yake ya kwanza kwasababu alikua na uchu wa kufanya kazi hiyo, pamoja na comment mbalimbali kutoka kwa wadau ambao wamekua wakimpa support katika kile anachokifanya.

Hata hivyo ameeleza sababu zinazowafanya mabinti wengi wanaojihusisha na fashion kushindwa kufika mbali ni kuwa wanawake wengi huwa wanaifanya kazi hiyo kama hobby na hawajali wanafaidika au hawafaidiki.

 “Unakuta msichana ana alternative nyingi ambazo zinamsaidia yeye kwenye maisha yake kiasi kwamba anakua anafanya fashion kama kitu anachokipenda haijalishi anafaidika au la,” anasema na kuongeza,

“Kwenye fashion sio kwamba mkiwa mia eti mkifanya vizuri haimanishi kuwa  wote  ndiyo mtachukuliwa hapana, kwani soko lake huwa linafanya selectiveness hivyo husababisha wachache ndiyo wanaofika mbali,” anasema.

Sambamba na hayo amesema kazi hiyo ina changamoto zake ambapo watu wanachukulia ukiingia kwenye fashion ni sawa na kupotea kwenye sanaa hiyo.

Vilevile anasema kuwa wakati mwingine mtu anashindwa kufanya kazi zake kutokana na ile perception hasa ukizingatia masuala ya kidini kuna baadhi ya mambo unashindwa kuyafanya.

 “Unaweza kutoa nguvu nyingi uka gain kidogo sana, lakini pia katika kutimiza malengo yako na kuishi katika maadili ya kidini hilo pia ni tatizo kwani naona jamii inaniangalia, familia hivyo baadhi ya mambo unashindwa kufanya”ansema

Aidha ameelezea namna anavyoweza kukabiliana na changamoto ya kazi yake hiyo kwa kutafuta shughuli nyingine ambazo zinaweza kumuingizia kipato, huku akihamasisha jamii na familia kuwa fashion ni kazi kama kazi nyingine.

“Im trying my little best katika kuielimisha jamii na familia yangu kuwa fashion ni kazi kama kazi nyingine kwa kuwatolea mifano ya watu ambao wamefanikiwa” anasema na kuongeza kuwa

Mabinti tunaoingia kwenye fashion basi tujitambue zaidi kuingia kwenye fashion sio sababu yaw ewe kutoka kwenye maadili yako muda wa kifashion ukifika unakua kama kazi inavyotaka na wakati mwingine wakua na familia ukiwadia basi unakua katika malezi yako kama kawaida”anasema.

Hata hivyo amesema soko la fashion kibongo bongo haliko vizuri kama ilivyo kwenye nchi nyingine kutokana na fashion ya bongo inakwenda kwa matukio.

 Vilevile anasema mfano hai unaonekana kwenye matukio ya Fashion hususani Swahili fashion ambayo hufanyika Disemba kila mwaka.

“kama ingekua kazi za fashion zinafanyiwa maonyesho kila mwezi tungefika mbali, yaani ili ufanikiwe lazima utumie nguvu kubwa ya kuhakiksha unaonyesha kazi zako kwa kiasi kikubwa ufanye photo shoot za kutosha ndo unaweza kufanikiwa”anasema.

Aidha amesema kwa sasa soko la fashion linakuwa kutokana na disaigner wanaongezeka, models wanaongezeka na kila mmoja anapambana kuandaa event yake na hawasubiri maadhimisho ya mwaka kufika.

Sambamba na hayo anasema kazi hiyo baada ya miaka kadhaa ijayo anategemea kuona mabadiliko makubwa hasa kwa upande wake kwa kushiriki maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Akielezea mafanikio aliyoyapata kupitia kazi hiyo anasema tayari ameshatengeneza platform nzuri ambapo hata mtu akioona picha yake sehemu yoyote basi ni rahisi kumtambua yeye.

Pia tofauti na fashion binti huyo anajihusisha na biashara ndogo ndogo ikiwemo uuzaji wa handbag, bites na anaitegemea elimu yake katika kuajiriwa na kujiajiri mwenyewe.

Malengo yako makubwa ni yapi?

“Kwanza nina mikakati yangu ambayo nimeiandaa kuachieve kila mwaka hususani kufanikiwa kimaisha, togive back to my community, familia yangu I want to archieve every strategies ambazo naziweka  kila mwaka”

Unawashauri nini mabinti wanaotaka kujiingiza kwenye fashion?

“kwanza wasivunjike moyo, watumie uniqueness zao ambazo wanazokuonyesha uwezo waliokuwa nao, japo mara nyingi kwenye masuala ya fashion jamii hua haitoi support yakutosha ila wanapaswa kupambania wanachokifanya”

Wewe ni binti mwenye misimamo ipi?

“Mimi ni binti ambaye very concistance ninaishi kwa principal na misimamo yangu binafsi”anasema

Mfahamu kwa ufupi Faraja Saidi

Faraja Saidi ni binti wa kwanza kati ya watoto wanne amezaliwa Mkoa wa Singida, na kufanikiwa kusoma primary katika mkoa huo huku Olever akasomea Tabora na Advance akafanikiwa kumaliza Arusha na kusoma Chuo jijini Dar es salaam akiwa anatarajia kumaliza mwaka huu.

 

 

 






Comments 6


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags