Fanya haya kutengeneza sauti yako kwa ajili ya kuimba

Fanya haya kutengeneza sauti yako kwa ajili ya kuimba

Zipo imani nyingi juu ya kutunza sauti kwa ajili ya uimbaji, wapo mwanaodai kuwa mayai na asali ni kati ya vitu muhimu katika kuboresha sauti ili iwe na mvuto.

Sambamba na hayo kila kitu lazima kiwe na mazoezi ili kiweze kuimarika, kama ilivyo kwenye baadhi ya michezo kama mpira wa miguu ambavyo wachezaji huzingatia mazoezi ndivyo pia inatakiwa kwa waimbaji au mtu anayetamani kuwa mwanamuziki.

Akielezea namna ya kuitunza sauti na kuifanya iwe bora Mwalimu wa Muziki kutoa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ‘TaSUBa’, Heri Kaare aliliambia gazeti hili kuwa mayai na asali si dawa ya kuwa na uwezo mzuri wa kuimba.

“Suala la uimbaji ni la mazoezi ya kuimba na siyo aina ya vyakula watu wanasema mtu ale mayai na asali hata ukila debe zima la asali halitokufanya uwe mwimbaji mzuri, kwa hiyo mwimbaji mzuri  ni zile hatua kwa sababu mwili unavyoimba unachukuaje hewa unaitunzaje, unafumbuaje mdomo na unaitumiaje mazoezi ya namna hiyo ndiyo yanasaidia mtu aweze kuimba kwa hiyo hivi vitu vingine nafikiri ‘vinasapoti’ lakini kuimba ni namna ya mazoezi anayopewa mtu ya kuimba vyakula ‘kusapoti’ koo lisiharibike lakini siyo kwamba  ndiyo vinafanya mtu aimbe,”alisema.

Alisema mtu yeyote mwenye uwezo wa kusikia ana uwezo wa kuimba pia “Mtu yeyote ana uwezo wa kuimba hasa awe na uwezo wa kusikia kwa sababu ili uimbe ni lazima uwe na uwezo wa kusikia, wapo wanaoshindwa kuimba licha ya kuwa wanaweza kuongea ni kwa sababu uwezo wa masikio kuwa mdogo,”alisema.

Vitu vya kuzingatia msanii kuitunza sauti

Mbali na mazoezi kwa ajili ya kuwa mwimbaji mzuri mwalimu huyo alieleza kuwa si vyema mwanamuziki kutumia vitu vyenye sukari nyingi kama vile soda, chocolate na pipi.

“Vitu vyenye sukari kama vile soda, pipi, chocolate siyo salama lakini pia siyo salama kutumia maji ya baridi.”

 
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags