Fanya haya kuepukana na unyanyasaji wa mitandaoni

Fanya haya kuepukana na unyanyasaji wa mitandaoni

Hellow! I hope mko good watu wangu wa nguvu, sasa leo najua utakuwa huna stress ukiwa unasoma habari hii kwasababu ni weekend kama mnavyoelewa watu wengi. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanawake hukumbana na unyanyasaji zaidi wa mtandao kuliko wanaume.

Waswahili walisema kunguru muoga huficha bawa lake na wengine wakasema mzaha mzaha hutumbua usaha, ni baadhi ya hekima ambazo zinaonyesha hatua ya kuchukua tahadhari katika maisha ya kila siku mitandaoni na kujiuliza nini uweze kukiweka mitandaoni na kipi ukiache kuhusiana na maisha yako binafsi.

Unyanyasaji wa mtandao ni kitendo cha kutumia teknolojia kumdhulumu mtu. Unyanyasaji huu wa mtandaoni unaweza kuhusisha moja au zaidi kati ya mambo yafuatayo:

kutuma maandishi au barua pepe za kuudhi, kuweka uwongo au matusi kwenye mitandao ya kijamii, na kushiriki video au picha za aibu mtandaoni. 

Vijana wadogo kwa mujibu wa takwimu za kimitandao ni kwamba wamekuwa wakikutana na ukatili mkubwa wa mtandaoni, hata baadhi wanafikia hatua ya kujiondoa uhai.

Kwa takwimu za nchi ya Marekani miaka mitatu iliyopita, waliliripoti watu 30 wanakufa kila siku kutokana na ukatili na udhalilishaji wa mtandao (cyber bullying).

 

Mwezi Oktoba uliomaliza umekuwa maalumu kwaajili ya kampeni na utoaji elimu kuhusiana na udhalilishaji wa kimtandao vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha maisha binafsi ya mtumiaji wa mitandao ama hata kujikuta taarifa zake zisizo za lazima kutolewa mtandaoni na kumpa wakati mgumu katika ubinafsi wake.

Yusuph Kileo, mtaalam wa usalama mtandao na uchunguzi wa makosa ya digitali ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa wana TEHAMA Tanzania, akizungumza na BBC alibainisha baadhi ya hatua za kuelimisha katika kujiepusha na mashambulio ya kimitandao alisisitiza kwamba matumizi sahihi ya kimtandao yanaanza na mtu binafsi,hivyo na kusisitiza kwa kila mtumiaji kuhakikisha kutuma taarifa na picha zilizo sahihi kimaadili na zenye ukweli.

Anasisitiza kwamba watumiaji wa mitandao wanawajibu kwa namna wanavyoweza kujilinda dhidi ya uhalifu wa kimitandao na namna ya kubaini changamoto za uhalifu wa kimitandao.

Pia mazingira ambayo yamekuwa yakiwatumbukiza watu katika majanga ya kutapeliwa mitandaoni;

Akizungumzia takwimu za ukatili wa kimitandao Yusuph aliiambia BBC kwamba watoto wenye umri kati ya miaka 12-17 asilimia takribani 37 wamekumbana na ukatili huo mitandao,

Hata hivyo akizungumzia msawazo wa kukumbumbwa na vitendo vya ukatili wa kimitandao,mtaalamu huyu alisema wanawake takwimu zinaonyesha ndiyo wahanga wakubwa wa kuathiriwa na changamoto mitandaoni ikilinganishwa na wanaume,ambapo wanawake wanarubuniwa kimapenzi (cyber romance)ama kudhalilishwa utu wao na vitendo vingine.

 

Wajibu unaanza na wewe mtumiaji

Katika kupambana na unyanyasaji na ukatili wa mtandaoni, Martha Evans, mtaamu wa usalama wa mtandaoni kutoka Uingereza, anashauri kuwa mambo mbalimbali ya kuzingatia ili kuwa salama kwenye matumizi yako ya kila siku ya mtandao.

Usijilaumu kwa kunyanyaswa mtandaoni, kitu chochote utachokiandika au kutuma kwenye mitandao yako, iwe picha, ujumbe au sauti majibu ya watu wa kwenye mtandao hayajasababishwa na wewe. Anasema Martha.

Lakini pia usijibu watu wenye lengo la kukunyanyasa kwenye mtandao, kuwajibu kunaweza kuzidisha zaidi na lengo lao likatimia.

Wewe mtumiaji unaweza kusababisha bila kujua’

 Watumiaji wengi wa mtandao wamekua na utaratibu wa kutuma mambo mbalimbali binafsi yanayowahusu kwenye mitandao.

Baadhi ya watumiaji huenda mbali zaidi na kutuma mambo ya faragha , ambayo kwa mujibu wa wataalamu kusababisha kufanyiwa unyanyasaji.

Kwa mujibu wa mkurugenzi msaidizi usalama wa mtandao wizara ya habari na mawasiliano ya teknolojia ya habari Nchini Tanzania Mhandisi Stephen Wangwe anasema watumiaji wamekua wakituma hadi vitu vya faragha katika mitandao.

‘’Lakini huu udhalilishaji unatokea katika angle kadhaa kadhaa,kuna wengine unakuta wamejipost wao wenyewe,wamejitafutia mazingira,wamejificha kwenye vyumba vyao halafu baadaye wameshare na dunia,sasa wanapokuwa wanashare na dunia hata kwa mujibu wa sharia ile ina mpa shida yeye  mwenyewe’’. Anasema Wangwe.

Je ni kwa kiasi gani kupakia kila kitu binafsi mtandaoni kinatoa mwanya wa mashambulizi kimitandao?

 Mwalimu Sammy Kissika katika mahojiano maalumu na BBC kuhusiana na usalama wa mitandaoni,anasema kwamba kwanza kabisa ni suala la mazoea yana tabu.

‘Mazoea yana tabu, mtu anaamka asubuhi anaweka picha sasa na kunywa,sasa nimekaa nje ya nyumba yako,sasa nafanya hiki na kile,ukiangalia kwa makini yale ni mambo binafsi ambayo yumkini hayana umuhimu wa kuyaweka hadharani unaweza usionekane haraka’lakini pia taarifa binafsi mfano hatimaye leo nimeweza kufungua  akaunti yangu mpya ya bank mfano akaweka na picha ya kadi mtandaoni,huyu ni rahisi taarifa zake za siri kuibiwa’’

"kwa sasa watumiaji wa mitandao wanaongezeka kwa kasi na pia ukiangalia ule muda wa kuweza kujifunza tahadhari za mitandaono haupo, mtu unauinua simu yako mpya leo,ama kifaa kingine cha mtandaoni,na kisha kuanza kuogelea katika uliwengu huo wa mitandaoni hapo hakuna muda wa simile tena hapo’’anasema Mwl Kissika.

 Hivyo kutokana na ukubwa wa tatizo hili ushauri wa kitaalamu kutoka kwa Yusuph Kileo mtalaam na mtafiti wa ukatili na udhalilishaji wa kimitandao ni kwamba,mtu anapokumbana na vitendo hivyo ni vyema kutoa taarifa ama kupitia mtandao anaoutumia ama kwa mamlaka husika kwa namba husika,lakini jambo jingine ni kwamba Pamoja na kuwepo mwezi maalumu wa kampeni na uelimishaji suala la kujifunza kuhusiana na usalama wa mitandaoni linapaswa kuwa endelevu, ikilinganishwa na madhara yanayosababishwa na udhalilishaji huo.

Lakini kwa wale ambao suala la kupakia vitu binafsi mitandaoni ni sehemu ya maisha ya kila siku haja ya kuhakikisha kwamba kunakuwa na hali ya kujizuia,ili kuepuka madhara yanayoweza kuwakumba.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags