Faida ya manjano katika urembo

Faida ya manjano katika urembo

Habari msomaji wetu, leo tunakutana tena ili kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala  ya urembo, mitindo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua zaidi.

Najua ni vigumu kueleza kinagaubaga maana halisi ya neno urembo ila naweza kusema kuwa urembo ni utumiaji wa mapambo, manukato, marashi, uturi, mavazi na rangi ili kuremba na kuongeza nakshi na umaridadi katika mwonekano.

Msomaji wa safi hii leo tutaangalia faida ya manjano katika urembo wa ngozi yako.

Manjano ni kiungo kinachotokana na mti uitwao Curcuma longa, mti huu unapatikana sana Kusini mwa bara la Asia, kiungo hiki kinatumiwa kwa namna nyingi.

Hata hivyo siku hizi mambo yamebadilika manjano ambayo yalikuwa ni kiungo muhimu katika chakula sasa hivi kimekuwa kiungo muhimu katika ngozi, yaani urembo wako unakuwa haujakamilika kabisa bila kutumia manjano hayo.

Ieleweke kuwa manjano mabichi ambayo hayajazimuliwa na sembe ndio mazuri hivyo epuka kutumia manjano yaliyochanganywa tayari na sembe.

Manjano yanaweza kukusaidia katika urembo  kutibu chunusi, kutokana na tabia yake ya kupambana na bacteria manjano yanauwezo wa kukausha chunusi hasa zile zinazotokana na maambukizi ya bacteria.

Kwa mwenye ngozi ya mafuta unachanganya manjano na maji ya waridi na wale wenye ngozi kavu unachanganya manjani hayo na maziwa freshi kisha unapaka usoni kwa nusu saa kisha unaosha na maji ya kawaida.

Pia manjano yanang’arisha ngozi, kama ujui manjano yanatabia ya kutoa weusi kwenye ngozi unaotokana na crimu, kuungua na jua au kufubaa kwa ngozi, unachotakiwa kufanya changanya manjano na maji ya waridi kisha sugua sehemu iliyoathirika.

Manjano pia inapunguza mafuta kwa wenye ngozi yenye mafuta pia usaidia sana kupunguza uzalishaji wa mafuta hapa utashangaa unachotakiwa kufanya ni kunywa glasi moja ya mchanganyiko wa maji na manjano angalau mara mbili kwa wiki.

Hata hivyo manjano upunguza kasi ya ngozi kuzeeka baada ya matumizi mengi ya vipondozi (make up), jitahidi kila mwisho wa wiki uwe unausugua uso wako kwa manjano angalau mara moja maana manjano haya usaidia ngozi isichoke haraka.

Natumaini kuwa kupitia hiki nilichokiandika wewe msichana unayependa urembo na ngozi yako utaweza kufuata ili kuhakikisha unakuwa maridadi na wa kuvutia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post