Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi

Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi

Na Shufaa Nassor

Hellow!!! I hope mko pouwaah, mimi kila siku niko hapa kuelekezana kuhusiana na maswala mazima ya Afya hususani ya wanawake, maana wengi wenu mnanitambua kama Madam hedhi salama, sasa leo katika  mwendelezo wa topic zetu tutazungumzia jambo ambalo kwasasa linatrenda sana kupitia mitandao ya kijamii. Kuhusiana na swala zima la saratani ya shingo ya kizazi.

Shingo ya kizazi (Cervix) ni kiungo cha mwili kinachopatikana kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke. Ni sehemu ya mji wa mimba (uterus) inayotokezea kwenye tupu (uke) wa mwanamke.

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Ni mabadiliko yasiyo ya kwaida ya chembechembe hai zilizopo kwenye shingo ya kizazi. Mara nyingi saratani hii ikiwa inaanza haionyeshi dalili yoyote hivyo mgonjwa hawezi kuchukua hatua yoyote kukabiliana na tatizo hili kwa wakati huu.

Kwa kiasi kikubwa saratani hii husabababishwa na maambukizi ya mda mrefu(Persistence infection) ya virusi waitavyo HUMAN PAPILOMA,  ambayo huenezwa kwa njia ya kujaamijiana.

Katika asilimia 99 ya visa, virusi vya HPV imegunduliwa kua kisababishi cha magonjwa ya zinaa hadi kwenye kizazi. Kuna takriban aina 100 za HPVS, kati ya hizo 16, 18 zinajulikana kwa kusababisha saratani ya shingo ya kizazi. Mara nyingi virusi hujuondoa wenyewe, kakini kwa asilimia ndoto 1-2%ya wa watu , huendelea na kusababisha saratani.

Kawaida mwili una uwezo wa hudhibiti maambukizi haya yaingiapo mwilini, lakini yasipodhibitiwa kikamilifu na  kuwepo mwilini kwa muda mrefu husababisha ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

MAMBO MENGINE YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

 📌Kufanya ngono zembe

📌Kuwa na wapenzi wengi

📌Kukoma siku katika umri mkubwa

📌Utumiaji matuta mengi katika chakula.

📌Kutokufanya mazoez ya mara kwa mara

📌Unene kupita kiasi

📌Uvutaji wa sigara

📌Utumiaji wa pombe kupita kiasi

📌Historia ya saratani ya matiti katika familia.

 

DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Dalili za ugonjwa huu huanza kutokea baada ya tatizo kuanza kukomaa, zifuatazo ni baadhi ya dalili;

✍🏻Kutokwa na maji ukeni

✍🏻kutokwa damu baada ya kujaamiana

✍🏻kutokwa damu isiyokua ya kawaida (damu isiyo ya hedhi)

✍🏻kuumwa miguu

✍🏻kizungu zunguna kuishiwa 

Nguvu 

UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI

HPV inachukua mda wa miaka 8-10  kubadili seli za shingo ya kizazi hadi seli zisizo za kawaida za saratani. Kwa havyo baadhibya vipimo vinapatkana ili kuona hali isiyo ya kawaida kwenye viseli, ambayo inayoweza kubadilika kuwa saratani.

Vipimo vya uchunguzi vinavyotumika sasa ni :

📌PAP SMEAR ; smear inachukuliwa kutoka kwa siveksi ili kuangalia isiyo ya kawaida ili kuangalia hali isiyo ya kawaida.

Inapaswa kuanzishwa katika umri wa miaka 30 au miaka 3 baada ya kujaamiana hadi umri wa miaka 65.

📌DNA YA HPV: inafanywa sana na smear ya pap lakini inachunguza HPV. Huanza akiwa na umri wa miaka 35 aidha akiwa peke yake au kwa smear kila baada ya miaka 5 hadi miaka 65. 

Ikiwa kuna hali isiyo yakawaida itagunduliwa katika mtihani huu na kisha  wanajikolojia watapendekeza kupata biopsy.

NINI KIFANYIKE??

Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika au kutibika kabisa endapi itagundulika ikiwa kwenye hatua za awali.

Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya yako kwa kadri utakavyoshauriwa na wataalam wa afya. 

Wanawake wote wanaoanzia umri wa miaka 30 na kuendelea wanatakiwa kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.

KUMBUKA:wakati wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni sasa, usisubiri hadi uone dalili, fika kituo cha huduma za afya kwa ushauri /mwongozo zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post