Fahamu uhusiano uliopo kati ya popcorn, Filamu

Fahamu uhusiano uliopo kati ya popcorn, Filamu

Imekuwa kawaida kwa baadhi ya watu kutaja movie kama sehemu yao ya starehe, tena wengine huenda mbali zaidi hutoka na kwenda sehemu maalum za kuoneshea movie kwa ajili ya kuburudika.

Wapo wa vibanda umiza ambavyo vipo kwenye mitaa mbalimbali , lakini pia yapo maeneo maalum ambayo watu huenda, yafahamikayo kama ‘Movie Theatres’.

Katima maeneo mengi ya ‘Movie Theatres’ ulimwenguni kumekuwa na tamaduni ya watu kuangalia movie huku wakila popcorn.

Sasa basi fahamu kuwa zipo sababu maalum zilizofanya kuwepo na mahusiano kati ya popcorn na movie.

Inaelezwa kuwa tangu miaka ya 1800, popcorn zilikuwa  ni vitafunwa maarufu, na ziliuzwa kwenye maeneo ya  sarakasi, maonesho na mitaani, wakati huo sehemu za sinema zikiwa hazijagunduliaka bado.

Sinema zilianza kuwa maarufu katika miaka ya  1900, na wakati huo popcorn bado zilikuwa hazijaanza kutumiwa kwenye kumbi za sinema.

Wamiliki wa kumbi hizo walijitahidi kufanya kumbi zipendeza kwa kuweka  viti vya kifahari na mazulia, lakini chakula chochote wakati huo hakikuruhusiwi katika kumbi hizo.

Hata hivo sinema kipindi hicho zilikuwa zikiangaliwa na watu wenye elimu na  matajiri kwani hazikuwa na sauti badala yake zilitegemea sana maandishi hiyo iliaminika watu wenye elimu ya kusoma ndiyo wangeweza kufurahi zaidi.

 Mwaka 1927 zilianza kutengenezwa sinema zenye sauti ambazo zilijumuisha watu wote zilikuwa zikitazamwa na watu wengi, hapo ndipo hekaheka za popcorn zikaanza.

Kutokana na watu wengi kuwa wanaigia kwenye kumbi hizo za filamu wauzaji wa mitaani waliona fursa na kuanza kuuza popcorn zao nje ya sinema na walipata wanunuzi wengi waliokuwa wakila nje.

Hatimaye, wamiliki wa kumbi za sinema waliona ni fursa kwao ya kutengeneza pesa na kuanza kuuza popcorn wenyewe.

Hivyo wamiliki hao waliona kutegeneza Popcorn si gharama kubwa lakini huleta faida zaidi, na hakuna ujuzi maalum unahitajika kuzitengeneza, pia harufu ya  popcorn ikageuka kuwa kuvituo.

Hapo ndipo wamiliki wa maeneo ya kuangalia sinema wakaanza kuzitengeneza na kuziuza. Na jambo hilo likawa kama tamaduni.

Kwa watazamaji nao walionesha kufurahia chakula hicho kwani hakizuii kutazama movie huku wanakula.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags