Kwa Tanzania na nchi jirani tumezoea kuona watu mashuhuri kukumbukwa yaani kuwa na siku zao maalum mfano, Nyerere Day, Karume Day, msanii na mfanyabiashara Roby Rihanna Fenty ambaye jina lake la kutafutia ugali wengi wanamfahamu kama Rihanna naye amefanikiwa kuwa na siku ambayo watu humuadhimisha.
Rihanna amezaliwa visiwa vya Barbados, kutokana na mafanikio yake ya biashara ya mavazi na muziki amepewa thamani kubwa katika Taifa hilo kwa kuwekwa siku maalumu ya mapumziko, ambapo Waziri Mkuu Mia Mottey, alimtangaza rasmi mwanamuziki huyo kuwa shujaa wa taifa hilo na kuweka siku maalumu ya kitaifa kwa kumpa heshima.
Licha ya kuwekwa siku hiyo vile vile katika mji huo kuna mtaa umepewa jina la ‘Rihanna drive’ kama heshima ya kulitangaza Taifa hilo #Duniani kupitia kipaji chake cha uimbaji na mitindo.
Hii imekuwa tofauti na msemo wa ‘nabii hakubaliki kwao’ maana Rihanna amejizolea umaarufu katika visiwa vya Barbados na ulimwenguni kote.
Aidha marekani kwenye makumbusho ya Metropolitan museum of Arts imechonga sanamu ya picha ya Rihanna kuonyesha ukubwa wake kwenye Tasnia ya Mzikii na Mitindo.
Haya sasa turudi kibongo bongo unafikiri msanii yupi anastahiri kupewa heshima kitaifa kupitia tasnia yake katika kuitangaza nchi ya Tanzania ulimwenguni, Shusha comment yako hapo chini.
Leave a Reply