Fahamu mambo yanayogusa moyo wa mwanamke

Fahamu mambo yanayogusa moyo wa mwanamke

Sasa hivi jamani wanaume wengi wanaamini kuwa wanawake, kwa kawaida wanapenda pesa na si kitu kingine.

Heti wanasema kwamba ukiweza kuhakikisha mwanamke wako anaweza kupata fedha kila anapohitaji basi unakuwa umemaliza kila kitu katikja mahusiano yenu.

Na fikra hizo kiukweli zimeleta mattaizo makubwa sana katika mahusiano ya vijana na hata kwenye ndoa pia.Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia.

Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.

Niwaweke wazi kuwa upweke huzaa migogoro isiyokwisha inayowafanya wanaume washindwe kuwaelewa wanawake. Kwa mtazamo wao, ni vigumu kumridhisha mwanamke. Wengine wanaenda mbali na kufikiri, 'mwanamke ni kiumbe mgumu kueleweka' kwa sababu, ‘hata ufanye nini...hata umpe nini hawezi kuridhika’.

Basi mimi leo nataka kuiondoa hizo fikra kwa kukuleta mambo ambayo naamini endapo utayafanya basi ni rahisi sana kuuguza moyo wa mwanamke.

Kwanza mwanamke anahitaji kuwa kipaombele chako, ndio mwanamke hatamani kuwa kwenye nafasi ya ‘mengineyo’, ‘ziada’, ‘baadae’ ‘nikipata muda’.

Unapomweka 'akiba' mwanamke hawezi kufurahia kwa sababu anatamani awe kipaumbele chako.

Unapokuwa na muda wa kuwa naye mara nyingi kadri inavyowezekana, kuahirisha mambo mengine ya muhimu kwa ajili yake, kuwasiliana naye kwa karibu na mambo kama hayo yanamdhihirishia kuwa ni kipaombele chako.

Nikwambie tu unaposhindwa kufanya hivyo, mwanamke hupata ujumbe kuwa yeye ni mtu wa ziada baada ya mambo ya muhimu.

Pili, mwanamke anapaswa kupendwa kwa vitendo jamani, Kumwambia tu unampenda bila kuthibitisha vitendo kuwa anapendwa hiyo inaweza kuleta shinda.

Kuna vitu kama zawadi, kutumia muda mwingi wa kupumzika pamoja na mpenzi wako, kutoka kwenda safari ya mbali na nyumbani hivyo ni moja ya vitendo ambavyo ukimuoneshea mwanamke atagundua kuwa unampenda.

Ila tunapaswa kutambua kuwa mwanaume kuambiwa anapendwa inaweza isiwe jambo la maana, lakini si kwa mwanamke. Mwanamke anatamani kusikia mara nyingi kadri inavyowezekana kuwa anapendwa.

Lakini pia mwanaume unapaswa kutambua ni vitu gani vya msingi ambavyo ukivifanya vitatuma ujumbe kuwa unampenda, nakwambia kama utashindwa kufanya hivyo mwanamke anaweza kujisikia kuwa hapendwi na hamu ya uhusiano inaweza kupotea.

 

 






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags