Fahamu kuhusu wito

Fahamu kuhusu wito

Ni matumaini yangu wazima wa afya kabisa, nafikiri katika pita pita zako umewahi kukutana na neno hili ‘Wito’ huku wengine wakitoa mfano kuwa uwalimu ni wito japo ni kazi kama kazi nyingine.

Kwa mujibu wa wikipedia inaeleza kuwa neno wito ni agizo au kaulimbiu inayotolewa na mtu au chombo kuhamasisha au kudai watu kuhusu jambo fulani.

Katika dini mbalimbali ni kama sauti kutoka kwa Mwenyezi Mungu inayomuelekeza mtu fulani afanye nini katika maisha yake, kwa mfano kutoa sadaka kwa watoto yatima nk.

Huku wengine wakieleza neno wito kuwa linawakilisha maslai binafsi, kile anachopenda, kinachomvutia, na kumsukuma mtu. Wito siyo kitu ambacho wewe unataka kufanya bali ni kile ambacho unahitaji kufanya.

Licha ya hilo wito nao unaweza ukakuingizia kipato au ukawa kazi pia. Na wito unaweza kuja kupitia maeneo mbalimbali kama vile sanaa, usanifu, au shughuli zozote zile za kiubunifu (kwa mfano; uandishi, uchoraji kufundisha, kutoa misaada, kukaa na watoto au wazee n.k.)

Mwananchi Scoop hatujakaa kinyonge tukaamua kuwatafuta watu mbalimbali ili kutuelezea kuhusiana na wao wana uwelewa gani kuhusiana na neno wito.

 Moja kwa moja tukamvutia waya mwalimu wa shule ya msingi Ken iliyopo Mbezi Msumi, Witness Mbua kwa upande wake yeye ameeleza kuhusiana na neno wito katika kazi yake ya Ualimu na kusema

 “Uwalimu ni wito kwa sababu ni kazi inayokutaka uwe na uweledi wa hali ya juu kufundisha mtoto asiyejua lolote ajue na aelewe unachomfundisha katika kazi ya ualimu wito ni kujitolea kwa hali na mali kwa kumfanya mwanafunzi kufaulu masomo yake” amesema Witness Mbua

Hatukuishia hapo tukakutana na mama mmoja aitwaye mama Mboga kwa upande wake yeye ameeleza kuwa yeye neno wito analieleza kufuatia biashara yake ya mbonga kwa kuesema

“Wito ni utayari wa kufanya jambo kwa hamasa kubwa kufahamu kazi unayofanya inamanufaa zaidi ya kipato, mfano mboga zinasaidia kila rika kuanzia watoto vijana na wazee na hata wamama wajawazito. Nikitazama kazi yangu hivi najua ni muhimu zaidi ya watu wanavyonitazamia na nafasi yangu ni kubwa kuliko kipato ninachokiingiza” amesema Mama Mboga

Huku na kule bwana tukakutana na Goodluck Beatus Ligogoderi ambaye ni Radiographer Zanzibar yeye amelizungumzia neno hilo wito ni sauti unayopewa na Mungu wewe binadamu na ndiyo maana kuna msemo ukasema kubali wito kata maneno.

Huku akiwataka watu kujitahidi sana kujua wito wao hapa duniani na uufuate hata kama watu watasema vibaya au kukukatisha tamaa zaidi

sana ni kuwa na amani, furaha na upendo wa kile unachokifanya au utakachokifanya kadri ya wito wako.

Kwa leo naomba tuishie hapo na nafikiri wale waliokuwa na ukakasi wameelewa kuhusu neni wito, ni jambo ambalo unaweza ukajitolea bila malipo lakini kazi unafanya kwa ajili ya kupata kipato, na wito pia unaweza kuufanya na kukuingizia kipato pia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post