Fahamu kuhusu kuachishwa kazi pasipo kufata utaratibu wa sheria

Fahamu kuhusu kuachishwa kazi pasipo kufata utaratibu wa sheria

Mambo vipi!!!wanetu sana najua mko swalama kabisa kama kawaida yetu sisi lengo letu mahususi kabisa ni kukuhabarisha ya usio yajua na unayo yasikia basi mwananchi scoop inakujuza zaidi au vipi mwanetu.

Leo katika kipengele cha kazi weekend hii tutazungumzia ni kwajinsi gani muajiriwa anapo achishwa kazi bila utaratibu wa kisheria mambo gani yanayotokea basi wewe ungana nasi mwanzo mpka mwisho.

kiujumla kuachishwa au kufukuzwa kazi kimakosa ni hatua ambayo mwajiri anamwachisha au anamfukuza kazi mwajiriwa wake bila kufuata utaratibu wa sheria.

Mwajiri asipofuata sheria katika kumuondoa mwajiriwa kazini ndipo anapokuwa amemwachisha kazi kimakosa.

Sheria yoyote haipaswi kuvunjwa au kukiukwa wakati mwajiriwa anapotakiwa kuachishwa kazi kwa hali yoyote ile mwajiriwa ana haki kujua au kufanya kitu anapo achishwa kazi bila utaratibu. 

KUNA AINA MBILI ZA KUACHISHWA KAZI KIMAKOSA.

  • Kuachishwa kwa kosa ambalo halipo

Hii ni pale ambapo mwajiri anamtuhumu mwajiriwa kwa kosa ambalo hajatenda kabisa, anamtungia kosa ili amuondoe kazini kwasababu anazojua mwenyewe.

Au inakuwa ni kweli mwajiriwa ametenda kosa lakini kosa lenyewe halina maana au uzito wa kumwondoa kazini, sio kila kosa ni la kumwondoa mtu kazini.

Makosa mengine ni ya kuonya au kuelekeza tu kwahiyo haya yakitokea ndipo tunaposema kuwa mwajiriwa ameachishwa kazi kimakosa kwa maana kwa kosa ambalo halipo au lipo lakini halitoshi kumuachisha mtu kazi. 

  • Kuachishwa kazi kwa kosa ambalo lipo lakini bila kufuata utaratibu.

Hapa kosa linakuwa ni kweli kabisa limetendwa na uzito wa kosa lenyewe unatosha kabisa kumuachisha mwajiriwa kazi. Tatizo linakuja kuwa wakati wa kumuachisha kazi kwa kosa hilo utaratibu unakiukwa kosa sawa lipo, lakini utaratibu wa kutumia kosa hilo kumwondoa mtu ndio uliokiukwa.


Utaratibu ni kama kutopewa taarifa yaani notice au kupewa taarifa lakini katika muda usiostahili, kutolipwa stahili, kutopewa nafasi ya kusikilizwa, nk.

Kwahiyo utaona tofauti ya aina hizi mbili za kuachishwa kazi kimakosa.
hata hivyo pamoja na utofauti huu bado unachostahili baada ya kuachishwa kazi kimakosa ni kilekile.

Aliyeachishwa kwa kosa ambalo halipo na aliyeachishwa kwa kosa ambalo lipo lakini kwa kukiuka utaratibu wote hustahili stahili sawa kama tutakavyoona hapa. 

UNACHOSTAHLI BAADA YA KUFUKUZWA KAZI KIMAKOSA.

Inapothibitika kuwa mwajiriwa (mfanyakazi) aliachishwa kazi kimakosa mambo yafuatayo yanatakiwa kufanyika ;

  • Kumrejesha mwajiriwa kazini .
  • Kulipa mishahara yake yote katika muda wote ambao hakuwa kazini.
  • Kumlipa posho zake zote, na malipo mengine ambayo yapo
  • kimkataba ambayo angelipwa kama angekuwa kazini.
  • Kumlipa mwajiriwa fidia kwa kumwachisha kazi kimakosa kwa kiwango cha mishahara isiyopungua miezi kumi nambili
  • Kutekeleza masharti mengine yaliyoamrishwa na mahakama ikiwa mgogoro ulifika mahakamani, au mliyokubaliana ikiwa mlifanya makubaliano.

Pia mahakama inaweza kuongeza kiwango cha malipo kwa namna itakavyoona inafaa. Hata hivyo stahihiki hizi zote unaweza kulipwa kwa kuelewana na mwajiri ikiwa mtaelewana au kulipwa kutokana na amri ya mahakama ikiwa mtakuwa mmefika huko.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags