Fahamu kijiji ambacho nyumba zao hazina ‘Milango’, Hakuna wizi

Fahamu kijiji ambacho nyumba zao hazina ‘Milango’, Hakuna wizi

Katika jamii nyingi ni vingumu kukuta wahusika wa nyumba wakiwa hawapo huku milango wameacha wazi, wengi wakitoka kwenda sehemu basi hufunga milango na madirisha yao ili kuepukana na wizi wa mali zao.

Lakini kwa upande wa kijiji cha Shani Shingnapur kilichopo nchini India imekuwa tofauti sana kwani nyumba zake huachwa wazi muda wote, kwani zimewekea uuwazi wa watu kuingia na kutoka ndani lakini hazina milango ya kufunga kama ilivyo sehemu nyingine ambazo hutumia milango ya mbao au chuma .

Kawaida milango ya  kijiji hicho haifungwi na wala hakuna mbao wala chuma kwa ajili ya kuziba kwani wanakijiji huamini kuwa wanalindwa na imani yao ,lakini pia katika kijiji hicho hakuna wizi kama sehemu nyingine.

Matukio ya kiharifu ya kuiba mali katika kijiji hicho hakuna watu huamini yeyote atakayeiba basi ataadhibiwa kwa imani yao kwa kupigwa upofu, huku mali za watu kama fedha zimekuwa zikiachwa ndani na hakuna anayechukua.

Si nyumba tu lakini hata katika milango ya maduka na  vyoo pia imetengenezwa kwa kufunikwa na kipazia chepesi, licha ya kuwa na imani hizo kituo cha polisi kilijengwa mwaka 2015 katika kijiji hicho ambacho pia mlango wa mbele upo wazi haufugwi,  na hakuna malalamiko ya uharifu yanayofikishwa kituoni hapo.

Kutokana na maisha wanayoishi wanakijiji hao imepelekea eneo hilo kuwa kivutio kikubwa nchini India kwani wakigeni kutoka mataifa mbalimbali humiminika kwa ajili ya kujione maajabu ya nyumba zisizo na milango.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags