Esha buheti amtolea povu Alikiba

Esha buheti amtolea povu Alikiba

Mambo yanazidi kinoga huko mitandaoni nah ii inatokana na msanii wa filmau nchini Esha Buheti kumtolea povu msanii wa bongo fleva Alikiba.

Unaambiwa juzi baada ya tukio la uzinduzi wa albamu ya Alikiba msanii huyo alianza kutoa shukrani kwa watu wake wa karibu pamoja na ndugu na jamaa waliohudhuria.

Kwa bahati mbaya aliwataja watu wote ila akamsahau muigizaji ambaye pia ni rafiki yake Esga Buheti hali ambayo imemfanya ajisikie vibaya

Hata hivyo kupitia InstaStory Alikiba aliamua kumuomba msamaha mwanadada huyo na kusema alijisahau na sio makusudi na kusisitiza kuwa Esha ni dada yake na yupo katika watu watu ambao ni wa muhimu kwake.

Baada ya kauli hiyo, kupitia Instagram ya Esha s Buheti aliandika kuwa “Mdogoangu sina tatizo na wewe kabisa na wala usiombe msamaha😪😪😪 mimi nimeona nipumzike tuuu na nlishasema nakupenda sana siwezi kukuchukia kua na Amani.

“Ali ukubwa jalala nayapokea yote nimeamua nikae pembeni maneno yamezidi hata mara mwisho nilikutumia msg nikakwambia Ali nimechoka na maneno ya watu na matusi mara najipendekeza mara sijui Ali hakusapoti mambo ni mengi sana so acha nibakie kua dada yako kama usemavyo na nisiwe shabikiako,” aliandika Esha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags