Eric Omondi kuingia live siku nne mfululizo bila kulala

Eric Omondi kuingia live siku nne mfululizo bila kulala

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya Erick Omondi ameeleza kuwa atatumia siku nne mfululizo bila kulala kuanzia siku ya leo Ijumaa saa mbili usiku hadi Jumatatu, ataingia live kwenye mtandao wa kijamii ili apate pesa ya kusaidia watu.

Eric amedai kuwa ndani ya siku hizo nne atazitumia bila kulala akiwa live na pesa atazopata kupitia mtandao zitaenda kusaidia wagonjwa nchini Kenya kupelekwa kupata matibabu India huku pesa nyingine itaenda kusaidia wafungwa na baadhi ya familia.

Atafanya hivyo kwani lengo lake kwa sasa ni kupata zaidi ya tsh 800 milioni. Unadhani Erick atatoboa siku nne mfululizo?

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags