Eric Omondi akubali kwenda gerezani kutumikia kifungo

Eric Omondi akubali kwenda gerezani kutumikia kifungo

Inadaiwa mshekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya Eric Omondi na wenzake wamehukumiwa kwenda jela kwa mwezi mmoja au kulipa faini laki moja na sabini.

Eric na wenzake hao 15 wamekutwa na hatia kwa kosa la kufanya mkusanyiko kupinga gharama za maisha bila kuwa na kibali.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mchekeshaji huyo kuna video inayoonesha akiwa na wenzake wakiingia mahakamani kusikiliza ‘kesi’.

Katika video hiyo imeambatana na ujumbe usemao, “leo mahakama imemuhukumu yeye na vijana aliyoongozana nao kwenda jela mwezi mmoja, huku akidai kuwa amehukumiwa kwa kupambana na gharama kubwa ya maisha”.

Hata hivyo mchekeshaji huyo aliongezea na kuandika kuwa yupo tayari kwenda gerezani kutumikia kifungo hicho cha mwezi mmoja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags