Eric Omondi adakwa na polisi Kenya

Eric Omondi adakwa na polisi Kenya

Mchekeshaji Eric Omondi anashikiliwa na maafisa wa usalama nchini Kenya, kwa kuongoza maandamano nje ya Jengo la Bunge.

Omondi alikamatwa baada ya kuongoza Mama wauza mboga katika maandamano hayo, kwa lengo la kupinga muswada wa fedha wa mwaka 2024. Baada ya kukamatwa kwake, mchekeshaji huyo alizuia katika chumba kilichopo ndani ya Majengo ya Bunge kabla ya maafisa kuanza kumhoji.

Licha ya kuwa mchekeshaji huyo alikamatwa lakini aliendelea kupaza sauti huku akijaribu kuhamasisha waandamanaji kuendelea na harakati hizo.

Katika video ambazo zimesambaa mtandaoni, zinaonesha waandamanaji wakiwa wameshikilia mabango makubwa huku wakipinga muswada huo.

Wakati wa maandamano, watu wengi walikuwa wanawake wakilaumu Bunge kwa udanganyifu huku wakidai kuwa walikuwa wakipanga kuidhinisha muswada wa fedha kuwa sheria.

Hii si mara ya kwanza kwa mcheshi huyo kukamatwa, Mwezi Februari mwaka jana, alikamatwa kwa kuongoza maandamano dhidi ya gharama kubwa ya maisha ambayo pia aliyafanyia nje ya Majengo ya Bunge.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post