Epuka Kuwaweka dawa watoto, Ipo Mitindo Mizuri ya Kuwasuka

Epuka Kuwaweka Dawa Watoto, Ipo Mitindo Mizuri Ya Kuwasuka

Habari za tangu wiki iliyopita msomaji mwananchiscoop najua u mzima wa afya na leo tunakutana tena ili kuweza kujuzana mambo mbalimbali uwenda unayajua lakini mimi nakujuza zaidi.

Leo napenda kukujuza juu ya mitindo mbalimbali ya nywele ambazo unaweza kumsuka mtoto wako wa kike akapendeza na ukaachana na kumuweka dawa za nywele kichwani kwake kwani si nzuri kiafya.

Najua kila mtu anapenda mtoto wake apendeze na hiyo ni mojawapo ya furaha kwao na leo nimeona ni vema nikuletee mitindo mbalimbali iliyo bomba kwa mtoto wako ambapo akisuka atapendeza badala ya kumuweka dawa ya nywele.

Nywele ndefu ni nzuri kwa watoto wa kike licha ya baadhi ya wazazi upendelea kuwanyoa watoto wao na wengine kuwasuka ila kwa mtoto anayependa kusuka ni vema akasuka mara moja kwa wiki au kwa wiki mbili na hiyo utegemea aina ya msuko atakaosukwa.

Si vema kumuweka mtoto wako nywele zake dawa kwani ubongo wake unakuwa bado ujakomaa na unaweza kumsababishia matatizo ya kiafya.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Janeth Jovin

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on business, money management on Tuesday and health on Thursday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include KARIA and FASHION.


Latest Post