Emoji kumi bora zilizotumika zaidi 2023

Emoji kumi bora zilizotumika zaidi 2023

Watumiaji wengi wa smartphones wamekuwa na utaratibu wa kuambatanisha jumbe wanazotuma na emoji mbalimbali, huku zikiwa na maana ya kuwakilisha hisia zao. Ikiwa zimebaki wiki mbili kuumaliza mwaka 2023 fahamu emoji kumi bora zilizotumika zaidi.

Tovuti ya Emojipedia imetoa emoji 10 bora zilizotumika zaidi ulimwenguni kwa mwaka 2023, ambapo emoji ya sura inayocheka hadi kutoa machozi ya furaha 😂 ikichukua nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na sura inayocheka hadi machozi huku ikijiviringisha🤣 .

Namba tatu kopa jekundu ❤️, nne mikono ya shukurani 🙏, tano sura inayotokwa machozi 😭, sita sura yenye kutabasamu huku ikiwa na kopa kwenye macho 😍, saba vimetameta ✨, nane emoji ya moto 🔥, tisa sura ya tabasamu 😊 , kumi sura ikitabasamu huku ikizungukwa na makopa 🥰.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags