Breel Embolo ni mchezaji wa Uswizi alifunga bao pekee dhidi ya Cameroon nchi aliyozaliwa katika mechi ngumu ya kwanza ya Kundi G ya Kombe la Dunia.
Embolo alikataa kusherehekea alipomaliza mashambulizi ya Uswizi punde baada ya kipindi cha mapumziko
Embolo alihamia Uswizi kutoka Cameroon pamoja na familia yake akiwa na umri wa miaka sita na alipewa uraia mwaka wa 2014.
Kabla ya mchezo huo alisema itakuwa ni tukio la kipekee sana kucheza dhidi ya Cameroon na alipofunga bao, aliinua mikono yake kwa heshima na kufumba macho.
Mashabiki kutoka Afrika wamekua na maoni mbalimbali kuhusu mshambuliaji huyo, wengi wakiuliza kuhusu baba yake anayeishi Cameroon na wengine wakifanya utani.
Leave a Reply