Elon Musk: Napenda mkilalamika kuhusu Twitter

Elon Musk: Napenda mkilalamika kuhusu Twitter

Mmiliki Mpya wa Mtandao wa Twitter, Elon Musk bado anaendelea kuwajibu na kuwakera watumiaji wa mtandao huo ambao wanalalamika kuhusu mchakato wake wa kutaka kulipisha dola 8 kwa kila akaunti yenye tiki ya bluu.

Elon Musk amemjibu mtumiaji mwingine wa mtandao huo ambae ameuita mchakato huo kama rushwa. Mmiliki huyo hakuamua kukaa kimya na kumwambia kuwa anapenda jinsi watu wanavyolalamika kuhusu Twitter hapohapo kwenye mtandao wa Twitter.

Mmiliki huyo aliandika, "I love when people complain about Twitter.... on Twitter, " na kumalizia na viiemoji vya kicheko.

Uwiiiiiiiih, siku zote waswahili tunakamsemo ketu bwana, upele umepata mkunaji, hahhaha! Ama Kweli Twitter Imepata mmiliki maana anajua kuwakera kama semaji la mabingwa.cool






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags