Elizabeth Mshana, Aeleza umuhimu wa tafiti kabla ya kuanzisha biashara

Elizabeth Mshana, Aeleza umuhimu wa tafiti kabla ya kuanzisha biashara

Kumekuwa na kundi kubwa la vijana ambao wanahitaji au amejiingiza katika ufanyaji wa biashara lakini uwenda wanakwama baada ya kushindwa kufanya utafiti wa kile wanachotaka au wanachokifanya.

Kuna msemo wa kiingereza umekuwa maarufu sana. Msemo huu unasema “Information is Power” yani “Kujua na kuwa na taarifa sahihi ya jambo ni Nguvu”.

Kila siku utasikia watu waliofanikiwa wakiongelea jinsi walivyoona fursa ya kuanzisha biashara fulani. Unafikiri waliwezaje kuiona hiyo fursa? Kiufupi ni kwamba walafanya utafiti katika biashara hizo walizoweza kufanikiwa.

Utasikia wengine wakisema baada ya muda fulani wakaongeza bidhaa kutokana na uhitaji wa bidhaa hiyo. Unadhani walionaje uhitaji huo? Utafiti ndiyo uliowasaidia kugundua hilo.

Utasikia wakisema wamefanikiwa kuongeza mauzo baada ya kutumia mbinu fulani ya kujitangaza. Wamejuaje kujitangaza kwa mbinu husika kunaweza kuwasaidia? Utafiti ndiyo kila kitu kwenye biashara.

Katika kudhihilisha hilo, Elizabeth Mshana huyu ni mshuari wa kibiashara ambaye anafunguka kuwa aliamua kufanya kazi hiyo baada ya kukutana na changamoto ya vijana wengi kutofahamu umuhimu wa tafiti kabla ya kuanzisha biashara.

Akifanya mahojano na mwandishi wa magazine hii, Mshana anasema kila anayetaka kufanya biashara anapaswa kuwa mtafiti ili ajue mambo ya muhimu yanayoendelea katika ujasiriamali na kamwe hutakosa fursa za kuingiza kipato milele.

Anasema utafiti mzuri katika biashara unaepusha upotevu wa rasilimali muhimu za biashara kama vile muda, juhudi pamoja na pesa na wateja.

Mshana amesema wajasiriamali wengi biashara zao zinakufa kwa sababu yakutofanya utafiti wakutosha juu ya biashara wanazoanza kufanya.

“Wajasiriamali wengi hawafanyi utafiti kwasababu ya kufanya biashara zao kwa mazoea kisa wanamuona mtu fulani anaifanya au amesikika akifanya biashara ya aina fulani na kafanikiwa na wewe unaamua kuingia mzimamzima bila ya kuifanyia utafiti wa kutosha biashara unayotaka kufanya,

“Kuna vitu muhimu vya kuzingatia unapofanya utafiti; chanzo cha mapato yako, gharama za biashara husika (mtaji), ushindani wa soko ulivyo, wateja wako ulionao, na bidhaa au huduma utakayoenda kuuza,” amesema.

Hata hivyo Mshana ambaye amesomea masuala ya Computer Application in Certificate na Secretary stage 2 katika Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (Veta), Dar es Salaam, amesema biashara ya ushauri anayoifanya nawasaidia vijana wengi kupata ushauri wa bishara gani anapaswa kufanya.

Pia amekuwa akiwashauri katika biashara hiyo ni wateja wa aina gani anaweza kuwapata na je usajili na vibali vya biashara vyake atavipataje na kuongeza kuwa yeye ni miongoni mwa watu wanaohusika na kufuatilia vibali hivyo kama mteja akiamua mumtumia.

Anafunguka na kusema alipata wazo la kufanya biashara hiyo mara baada ya kukutana na changamoto wakati akimuombea chuo na cheti cha kuzal;iwa mdogo wake.

“Hapa nilipata changamoto na ndio nilipoona fursa maana ni wengi wanaoteseka kufanya biashara hii, changamoto nyingine ni ile ambayo tumeeleza hapo juu ya watu kutofahamu umuhimu wa kufanya utafiti wa biashara kabla ya kuanza,” amesema

Faida anazozipata

Amesema moja ya faida anazozipata anajifunza mengi kupitia kwa wateja wake, kupata marafiki wapya pamoja na fursa za biashara mbalimbali zilipo nchini na nje ya nchi.

Ushauri wake

Amesema ushauri wake kwa vijana ni uhakikisha wanageuza changamoto kuwa fursa.

“Ndio changamoto unazokumbana nazo hakikisha zinakupa fursa ya kufanya biashara au wazo la kufikiria kitu gani ufanye ili ujiingizie kipato cha kujikimu na maisha ya kila siku,” anasema

Aidha anasema kitu kingine ambacho anapenda kufanya ni kujifunza kila mara na kupika.

Kuhusu familia

“Mimi ni mama wa mtoto mmoja, mtoto wangu amefanyika baraka mno. Kila siku Asubuhi lazima nimuandae na kumpeleka shule na jioni nimuangalie masomo yake. Lakini weekend jumamosi na jumapili ni siku yangu ya kukaa na familia,” anasema Mshana

Hata hivyo Mshana anasema anatamani kuwa kama Jenipher Bash maarufu kama mama Alaska na Aunt Sadaka.

“Natamani kuwa kama Mama alaska na Aunt Sadaka kwasababu wao ni wanawake, na mama wa familia lakini wanamiliki biashara zao na zinafanya vizuri sana. Najifunza mengi kupitia kwako ikiwemo heshima ya kazi, kufanya kazi kwa juhudi, na kulinda brand yako,” anasema Mshana

 


Comments 3


 • Awesome Image
  Baraka Jeremia

  Ushauri wako mzuri Sana kwa vijana tunaoanza biashara Ni hakika utafiti wa Biashara husika Ni muhimu Sana 🙏 ubarikiwe sana 👍🙏

 • Awesome Image
  Lulu

  Nice madam 👏👏

 • Awesome Image
  Lulu

  Nice madam 👏👏

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post