Dullah Mbabe kuzichapa leo Tunduru

Dullah Mbabe kuzichapa leo Tunduru

Mambo ni moto huku wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwani Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' amewasili tayari kwa ajili ya pambano lake maalum la Kimaonyesho linalotarajia kupigwa leo.

Dullah Mbabe atapanda ulingoni kwenye pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa CCM Wilayani hapo lengo likiwa ni kuhamasisha ngumi mkoani hapo pamoja na kupata mabondia watakaopanda ulingoni katika pambano la Seleman Kidunda dhidi ya Tshimanga Katompa ambalo linatarajia kupigwa Julai 30, mwaka huko Songea.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Tunduru ambapo amepokelewa na shangwe la mashabiki, Dulla Mbabe amesema kuwa hakutegemea kama angeweza kupokelewa kwa shangwe hilo hivyo ana deni kubwa kwao ambalo ni kuwaonesha mchezo mzuri katika pambano lake la leo dhidi ya Ramadhan Migwede.

"Nimekuja kucheza katika hili pambano kwa lengo la kuhamasisha ngumi hapa kwa sababu ngumi zinapaswa kuwepo mikoa yote nchini siyo baadhi ya mikoa, namshukuru promota kwa wazo hili ila niwaombe mashabiki wangu wa hapa Tunduru mje kwa wingi kuangalia burudani kutoka kwangu," amesema Dullah Mbabe.

Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni kwenye pambano hilo linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Wilaya ya Tunduru kwa kuwakutanisha Chidy Benga wa Songea dhidi ya Yazidu Khalfani wa Tunduru wakati Matumla Matumla wa Tunduru akitarajia kumvaa Azizi Azizi wa Songea.

Wengine ni Karim Mwenda wa Songea atakayecheza na Giliki Giliki wa Tunduru wakati Bashiru Kazembe atacheza na Kapinga, Seleman Khalifa vs Judi Rajabu, Julo Julius vs Mwakinyo Mbabe wote wakiwa ni wa Tunduru wakati  Kachala Mnyama yeye atacheza dhidi ya Junior kutoka Malawi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post