Dulla Makabila awaomba msamaha Wanasimba

Dulla Makabila awaomba msamaha Wanasimba

Mwanamuziki wa singeli Dulla Makabila amewaomba radhi mashabiki wa Simba huku akiomba waridhie aweze kutumbuiza katika tamasha la ‘Simba Day’ linalitarajia kufanyika Agosti 3 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Makabila ameomba msamaha huo wakati alipokuwa akisubiri uzinduzi wa treni ya umeme akiwa na wasanii wenzake Lulu Diva pamoja na Alikiba akidai kuwa hatorudia kuwasema vibaya tena.

“Naomba mnisamehe sana wanasimba ni mambo ya pombe tu siwezi kuongea tena kama vile naomba mnisamehe sana” amesema Makabila

Ukiachilia mbali kuomba msamaha huo leo siku ya jana Julai 31 aliachia kionja cha wimbo unaotarajiwa kutoka leo saa nane mchana ambao ni mahususi kwa ajili ya kuwaomba radhi wanasimba.

Utakumbuka kuwa siku ya jana moja ya taarifa zilizosambaa zaidi ni kuwa jina la Dulla Makabila limekatwa na hatoweza kuungana na wasanii wenzie katika kutumbuiza kwenye tamasha la ‘Simba Day’.

Wasanii ambao mpaka sasa majina yao hayajakatwa na wanauhakika wa kutumbuiza Simba Day ni Joh Makini, Alikiba na Chino Kidd.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags