Drake kufikishwa mahakamani

Drake kufikishwa mahakamani

PosKampuni ya Wanamitindo ya ‘Members Only’, imefungua kesi dhidi ya kampuni ya Drake, ‘Away From Home Touring Inc’, katika mahakama ya shirikisho ya New York kwa madai ya kukiuka alama za biashara.

Hatua hizo za kisheria zinachukuliwa dhidi ya Drake baada ya kutumia maneno yaliyopo kwenye bidhaa za ‘Members Only’ katika ziara yake.

Drake aliuza bidhaa hizo katika mitandao ya kijamii pamoja na kuziuza kwenye ziara yake ya ‘It's All a Blur’ huku akituhumiwa kuuza bidhaa zisizo za halali na kutumia neno hilo ‘Members Only’ kama jina la wimbo wake uliyopo kwenye album ya ‘For All The Dogs’ iliyotoka rasmi mwaka jana.

‘Away From Home Touring’ pia ni ziara ya kwanza ya msanii huyo kutoka Canada ilianza Aprili 5, 2010 huko Slippery Rock, Pennsylvania na kutamatika Novemba 6, 2010 jijini Las Vegas.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags