Drake afurahishwa kuachiwa huru kwa Vybz Kartel

Drake afurahishwa kuachiwa huru kwa Vybz Kartel

‘Rapa’ Drake ameonesha furaha yake baada ya mkali wa Dancehall kutoka Jamaica, Adidja Palmer ‘Vybz Kartel’ kuachiwa huru kutoka jela baada ya kusota kwa miaka 13.

Drake kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha ya staa huyo huku ikiwa na ujumbe uliyokuwa ukisomeka “Boss free up now” akiwa na maana ya Bosi yupo huru sasa.

Siku ya jana Jumatano Julai 31, Mahakama ya Rufaa ya Jamaica iliamuru kutosikilizwa kwa kesi ya Vybz Kartel kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo kiafya inayotishia uhai wake ambapo ilibainika kusumbuliwa na maradhi ya ‘Graves’ Disease’ yanayosababisha matatizo kwenye koo, moyo na saikolojia yake.

Staa huyo ambaye aliwahi kushirikiana na wasanii wakubwa kama Jay-Z na Rihanna katika harakati zake aliswekwa jela tangu mwaka 2011 baada ya kukamatwa kufuatia na mfanyakazi mwezake Clive “Lizard” Williams kutoweka ambapo mpaka kufikia sasa mwili wake haujawahi kupatikana.

Utakumbuka kuwa Kartel alihukumiwa kifungo cha maisha jela Machi 13, 2014 baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya Clive ‘Lizard’ Williams akishirikiana na wenzake watatu ambao ni ‘Shawn Campbell’, Andre St John Na Kahira Jones






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags