Drake afunguka kuacha muziki ili azingatie afya yake

Drake afunguka kuacha muziki ili azingatie afya yake

Muda mchache kabla ya kuachia albamu yake mpya ‘For All The Dogs,’ siku ya jana Drake alitangaza kuwa huenda akaachana na muziki kwa muda kidogo ili aweze kuzingatia afya yake.

Wakati akiwa kwenye kipindi cha redio, "Table For One" kwenye SiriusXM's Sound 42, rapper huyo amesema kuwa ana matatizo ya tumbo ambayo amekuwa akikabiliana nayo kwa miaka mingi.

Hivyo basi katika mazungumzo hayo Drake akaongezea kuwa huenda akasimama kwa takriban mwaka mmoja kwa ajili ya kujiweka sawa na kuzingatia afya yake. Albamu yake mpya aliitoa siku ya jana Ijumaa ikiwa na nyimbo 23.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags