Dora akanusha kuzaa na Mchungaji

Dora akanusha kuzaa na Mchungaji

Baada ya kuzuka uvumi kupitia mitandao ya kijamii ikieleza kuwa watoto watatu wa mchezaji wa ‘timu’ ya taifa ya Nigeria, Kayode Olarenwaju kuwa siyo wake, aliyekuwa mke wa mwanasoka huyo Dora Ezinne amekanusha uvumi huo.

Dora alikanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kudai kuwa Kayode aliamua kusambaza taarifa hizo kutokana na kuwa na hatia ya kuwanyanyasa watoto hao ambapo Dora amemtaka Kayode kuonesha majibu hayo ya DNA hadharani na kutaja jina la hospitali aliyofanyia uchunguzi na yeye yupo tayari kufanya DNA ya watoto hao.

Ikumbukwe kuwa uvumi huo ulianza kuzuka siku mbili zilizopita ukidai kuwa watoto watatu wa Kayode Olarenwaju siyo wake huku majibu ya vipimo hivyo yalibainishwa kwamba watoto ni wa mchungaji ambaye Dora alikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.

Hata hivyo kwa mujibu wa mchungaji anayetuhumiwa na sakata hilo aitwaye Tobi amefunguka kupitia mitandao yake ya kijamii kwa kueleza kuwa,

“Waacheni watoto wangu waje nyumbani, kila mtoto anastahili mazingira mazuri ya kukua, siyo yenye sumu, watoto wanahitaji baba na siyo mtu wa kuwatisha”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags