Don Jazzy amkataa Wizkid instagram

Don Jazzy amkataa Wizkid instagram

Mwanamuziki na mmiliki wa Lebo ya ‘Mavin Records’ kutoka nchini Nigeria, DonJazzy amem-unfollow msanii #Wizkid katika mtandao wa #Instagram baada ya msanii huyo kujibu tweet ya ‘rapa’ #Ladipoe kuwa hazungumzi na wasanii waliosainiwa na ‘Influencer’ ambaye ni Don Jazzy.

Jana rapa #Ladipoe ambaye ni msanii wa Mavin Records ali-tweet kuwachana wasanii wa Afrobeat ambapo aliandika:

“Nigerian rappers that survived (hiphop is dead), watching afrobeats artist going through their own”

Hivyo kupitia ujumbe huo shabiki mmoja aliujibu kwa kumuita Wizkid aje aingilie tweet hiyo, na wizkid alijibu kamwe hazungumzi na yeyote aliyesainiwa na influencer’ (alimaanisha Don jazzy)

Hata hivyo mashabiki wengi wamemjia juu Wizkid wakidai kuwa amemkosea heshima Don Jazzy kwa kumuita ‘influencer’, huku wengine wakipinga suala hilo na kusema kwamba msanii huyo hana kosa lolote

Don Jazzy aliwahi kushinda tuzo mbili mfululizo kama ‘music influencer of the year’ katika tuzo za pulse mwaka 2023 nchini humo.

Ikumbukwe mwaka 2022 Wizkid aliwachana rappers wa nchi hiyo na kusema kwamba hasikilizi muziki wa Hip-Hop kwasababu unaboa, hauna ubunifu, beat ni zilezile, hakuna kitu kipya na kudai kuwa Afrobeat ndiyo muziki bora duniani kwa sasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags