Dk. Dre kumlipa Nicole bilioni 230

Dk. Dre kumlipa Nicole bilioni 230

Producer kutokea pande za Marekani  DK. Dre, rasmi sasa wamefikia makubaliano ya kuvunja ndoa yake na aliyekuwa mke wake Nicole Young japo atatakiwa kumlipa mwanadada huyo kiasi cha Milioni 100 za Marekani ambazo ni sawa na Bilioni 230 za Kitanzania.

Kwa mujibu wa TMZ Producer huyo pamoja na mke wake wamefikia makubaliano hayo na mke wake waliodumu takribani miaka 24 kuachana rasmi kisheria.

Nicole atapokea Dola Milioni 50 sasa na nyongeza ya dola Milioni 50 ndani ya mwaka mmoja ambayo ni sawa na malipo ya Dola Milioni 100 kwa pamoja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags