Dk. Death azindua mashine ya kutoa uhai kwa wanaotaka kujiua

Dk. Death azindua mashine ya kutoa uhai kwa wanaotaka kujiua

Shirika la Exit International kutoka nchini Marekani ambalo lipo chini ya Dk. Philip Nitschke, maarufu kama ‘Dr. Death’ limevumbua sanduku maalumu la kujiua liitwalo ‘Sarco Pod’ au ‘Kibanda cha kujiua’.

Sarco Pod ni mashine ambayo inafanya mtumiaji afurahi na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja kabla ya kuaga dunia, hata hiyo imedaiwa kuwa sanduku hilo halisababishi maumivu wakati mtumiaji anapotaka kujiua.

Aidha CEO wa kampuni hiyo Dk. Philip Nitschke, alieleza kuwa kabla ya kuchukua hatua ya kujiua mashine hiyo inamuuliza maswali matatu mtumiaji, ambayo baada ya kuyajibu atabonyeza kitufe kilichopo ndani ya sanduku na atajiua.

Maswali hayo ni kama ‘Wewe ni nani?, ‘Uko wap?, na Je unajua kitakachotokea ukibonyeza kitufe?

Una maoni gani kuhusu hili?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags