Djokovic : sipingi chanjo ila sitachanja

Djokovic : sipingi chanjo ila sitachanja

Ebwana hii nayo ni kubwa kuliko Nyota wa Tennis Mserbia Novak Djokovic amesema yupo tayari kukosa michuano mikubwa ijayo ya tennis(French open na Wimbledon open) lakini hayupo tayari kuchanjwa kama ilivyokuwa kwenye michuano ya wazi ya Australian 2022 yaliyomalizika mjini Melbourne mwezi January 31.

"sijawahi kupinga chanjo hata siku moja kwa sababu nilipokuwa mdogo nilipata chanjo kadhaa,lakini kila siku naunga mkono uhuru wa mtu kujiamulia kitu gani kiingine kwenye mwili wake na nipo tayari kulipa gharama ya kutoshiriki kwenye mashindano yajayo kisa kubaki na msimamo wangu wa kutochanjwa "amesema Djokovic

Djokovic mwenye umri wa miaka 34, anayekamata nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango wa tennis duniani kwa upande wa wanaume huku akiwa na mataji makubwa 20 ya tennis (Grand Slams) alizuiliwa kushiriki kwenye michuano ya wazi ya Australian mwaka 2022 baada ya kuzuiliwa kutokana na kutochanjwa chanjo ya Uviko 19 na kunyang'anywa pasi yake ya kusafiria ya kuingia nchini humo.

Novak Djokovic amesema anaamini vigezo vya chanjo kwenye mashindano makubwa yanayokuja yatarekebishwa na kuwa na matuamaini ya kushiriki kwenye michuano hiyo tena kwa miaka mingi ijayo ya mbeleni na kusisitiza anataka kuweka rekodi kubwa kwenye mchezo huo huku tayari nyota kutoka nchini Hispania Rafael Nadal akiwa na mataji 21 na kuwa mcezaji wa tennisi mwenye mataji mengi kwenye historia ya mchezo huo duniani.

Unaweza kutoa maoni yako mdau juu ya suala hilo je unamshauri nini Djkovic tuambie kupitia www.mwananchi scoop.co.tz.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post