Dj Stivie j aendelea kumkingia kifua Diddy

Dj Stivie j aendelea kumkingia kifua Diddy

Baada ya nyaraka za kesi zilizofunguliwa na mtayarishaji Rodney Jones dhidi ya Diddy zikidai kuwa Party zinazofanyika nyumbani kwa Combs zimekuwa zikijikita katika biashara ya ngono, sasa Dj na producer Stivie J amekanusha suala hilo kwa kuposti video ya party inavyokuwa kwa Diddy.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Dj Stevie J ame-share video hiyo ya moja ya party ambazo zinafanyika nyumbani kwa Diddy kila mwaka ikiambatana na ujumbe usemao “Hivi ndivyo Diddy Party halisi inavyoonekana”.

Ikumbukwe kuwa wiki moja iliyopita makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami, ambapo ndiyo hufanyika sherehe hizo yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post