Dj Mosso Misondo ni upepo tu

Dj Mosso Misondo ni upepo tu

Kwenye tasnia ya burudani anaye-trend sasa ni DJ Misso Misondo ambaye kwa sasa ‘upepo’ umemgeukia na kila kona unayopita lazima utamsikia,'Umepigaje hapo'. Misso amefunguka kuwa hajasomea UDJ lakini kupitia kujitafuta akajikuta anafanya kazi hiyo na hadi sasa ana zaidi ya miaka miwili akipiga ngoma Kanda ya Kusini lakini kwa sasa ndiyo amekuwa maarufu Tanzania.

“Wakati wa Mungu ndiyo wakati sahihi. Nimekuwa nikipiga muziki huko Kusini na wengi wananitambua lakini katika maeneo mengine nadhani walikuwa hawajazingatia kama ilivyo sasa, nadhani huu ndiyo muda sahihi na mimi nipo tayari kupambana kwa muda wowote ili Watanzania wafurahi,” amesema Misso Misondo.

Aidha Misso ameweka wazi namna alivyokutana na madansa wake ambao staili yao ni kuvaa makoti makubwa machafu na kuunda timu.

“Wale jamaa tulijuana kwenye show moja ambayo mimi na wao tulialikwa tukafanye kazi kila mmoja kimpango wake, baada ya kuona tunaendana ikabidi tuanze kufanya kazi kwa pamoja. Nawakubali na siwezi kuwaacha,” Amesema Misso.

Hadi sasa Misso Misondo amefanya ngoma na star wa Bongo fleva, Rayvanny iitwayo ‘Kitu Kizito’, na tayari amehamia Dar es Salaam kutoka Mtwara baada ya kupata shavu katika moja ya vituo vya redio vya jijini Dar es Salaam.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags