Diva, Nimechoka kesi za wanawake zimekuwa ni nyingi

Diva, Nimechoka kesi za wanawake zimekuwa ni nyingi

 

Heheheh! Jamani jamani waswahili wanasema ndoa isikie kwa mwenzako ila usijalibu kukurupuka, basi bwana mtangazaji Diva theebawse amefunguka ya moyoni kuhusiana na changamoto amabazo anakumbana nazo katika ndoa yake.

Divatheebawse amefunguka hayo kupitia instastory yake na kueleza kuwa “kesi za wanawake nyingi mechoka ati, nilifikiri ndoa mtu akiwa mke anaheshimika lakini ndoa yangu inakuwa ya kushambuliwa na wanawake kila kukicha kulala walale wao matusi kwangu inahusu?” amesema Divathebawse

Aidha mwanadada huyo aliendele kwa funguka kwa kusema “Sielewi mpaka dakika hii kwanini wananiingiza katika ujinga wao so ule upole kwangu saa hii sina naona heshima eti niliolewa kwa heshima sikuokotwa mimi ni mke halali mpaka tukishindwana labda na kama kuna mtu alikuwa nae huko siyajui Sielewi Why wananikosea heshima kiasi hiki” amesema Divathebawse

Haya sasa wale mnapenda kufuatilia ndoa za watu jamani mnafanya watu watokwe na makovu hahaha! Wadau wa Mwananchi Scoop embu dondosha komenti yako hapo chini nawewe utoe povu lako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags