Diva: Awali sikujua kama Abdul anamke

Diva: Awali sikujua kama Abdul anamke

Nyieeee ukisikia balaaa ndio hili sasa bwana Mtangazaji maarufu nchini Tanzania Divatheebawse amefafanunua kuhusu tetesi za kuingilia mahusiano ya mtu.

Diva ameamua kufunguka kupitia mahojiano aliyofanyiwa na kituo kimoja cha television hapa nchini kwa kukanusha taarifa ambazo zilisambaa mitandaoni awali kuwa aliolewa na Sheikh Abdulrazak Salum ilhali anafahamu kuwa mwanaume huyo alikua ameoa.

Diva amekanusha tetesi hizo na kuweka bayana kuwa hakufahamu kama mume wake huyo alikua ameoa hapo awali.

Aidha Diva aliendelea kwa kusema kuwa hakufurahishwa na matokeo hayo baada ya kufahamu kuwa mume wake ameoa na hivyo alimwambia achague moja kwani yeye hakuwa tayari kuwa mke wa pili na pia hakupenda maneno yaliyokua yanaendelea kwenye mitandao ambayo anasema yalikuwa yanamchafua sana.

 








Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags