Diva: Abdul hakufuata pesa kwangu

Diva: Abdul hakufuata pesa kwangu

Baada ya tetesi kua nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mume wa Divatheebawse amefata pesa kwa mrembo huyo hatimaye Diva amenukanusha taarifa hizo.

Diva amefunguka na kusema kwamba mume wake Sheikh Abdulrazak Salum hajafuata pesa kutoka kwake kwani hata wakati wanatarajia kufunga ndoa yao, Mume wake huyo ndiye aliyekuwa akitoa hela kwa ajili ya kugharamia vitu mbalimbali kwa ajili ya ndoa yao hiyo.

“ Sio kweli kwani nakumbuka hata wakati alipokua akitaka kunioa yeye ndiye alikua anatoa fedha” alisema Diva

Hata hivyo  Divathebawse Aidha, amesema kwamba uhusiano kati yake na mume wake ni 50/50 ikiwa na maana kwamba wao wanaishi kwa kutegemeana, endapo kuna jambo Divathebawse anaweza kufanya atafanya na endapo hawezi basi Sheikh Abdulrazak  ambaye ni mume wake atafanya na hivyo ndivyo jinsi wanavyoishi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags