Director Wa Wakanda Forever Aweka Historia Marekani

Director Wa Wakanda Forever Aweka Historia Marekani

Mtayarishaji na mwongozaji wa filamu nchini Marekani, Ryan Coogler ambaye alipata umaarufu kupitia filamu ya ‘Wakanda Forever’ ameweka historia kuwa mtayarishaji wa kwanza mweusi kuwa na filamu nne zilizopata zaidi ya dola milioni 100 (Sh 256 trilioni).

Kwa mujibu wa tovuti ya Black Filmandtv’ Coogler ameweka historia hiyo kupitia filamu zake kama Creed (2015) iliyoingiza mapato dola 109 milioni, Black Panther (2018) ikiingiza dola 700 milioni, Black Panther: Wakanda Forever (2022) ikipata dola 453 milioni pamoja na Sinners (2025) ambayo imefanikiwa kuingiza dola 122.53 milioni ndani ya siku tisa.

Kutokana na mafanikio hayo mtayarishaji huyo anatajwa kuwa mmoja wa waongozaji bora wa filamu ambaye amewanyanyua Waafrika na Wamarekani Weusi katika tasnia ya filamu ya Hollywood.

Kabla ya kuingia katika uandishi wa filamu Coogler alitamani kuwa mchezaji wa mpira wa miguu (football), lakini kipaji chake cha uandishi na hadithi kilianza kung'aa akiwa chuoni.

Alianza kutambulika kupitia filamu yake ya kwanza ‘Fruitvale Station (2013)’ ambayo ilimletea sifa kubwa. Filamu hiyo ilieleza kisa cha kweli cha Oscar Grant, kijana mweusi aliyeuawa na polisi mjini Oakland. Filamu hiyo ilishinda tuzo nyingi, ikiwa ni pamoja na tuzo kubwa katika Tamasha la Filamu la Sundance.

Kwa sasa, Ryan Coogler anatamba na filamu yake mpya ya kutisha iitwayo Sinners, ambayo imepokelewa kwa shangwe na mafanikio makubwa ambayo imecheza na wahusika kama Michael B. Jordan, Miles Caton, Jack O'Connell, Wunmi Mosaku, Hailee Steinfeld, na Delroy Lindo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags