Dili la kupika tambi za mayai

Dili la kupika tambi za mayai

Yees!! Mambo vipi mtu wangu karibu kwenye ukurasa wa nipe dili kama kawaida hua tunapeana madini mbalimbali kuhakiksha mambo yanakwenda sawa bin sawia.

Leo kwenye nipe dili nataka kukujuza zaidi jinsi utakavyoweza kuandaa na kupika tambi za nyama, aisee umewahi kula utamu huu? karibu tupike kwa pamoja.

MAHITAJI.
Tambi ½ paketi.
Vitunguu maji 2 vikubwa.
Karoti 1.
Hoho 1.
Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula.
Carry powder kijiko 1 cha chai.(sio lazima)
Njegere zilizochemshwa ½ kikombe.(sio lazima)
Mafuta kwa kiasi upendacho.
Mayai 2.
Chumvi kwa ladha upendayo. 

JINSI YA KUNZA MAPISHI


1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu.


2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni.


3. Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.


4. Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .


5. Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.

Tayari kwa kula,ukitaka tambi zako zisivurugwe yaani ziwe kama kwenye picha , ukiongeza mayai usizigeuze hadi unapoona yai limeiva kwa chini unageuza upande wa pili kama upikavyo chipsi yai.

Naam!!! Hivyo ndivyo mambo yatakavyokuwa wakati unapika tambi zako nafikiri tumefahamiana vizuri kabisa enjoy msosi mtamu!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags