Diddy na kampuni ya Diageo wamaliza tofauti zao

Diddy na kampuni ya Diageo wamaliza tofauti zao

Baada ya kurindima mahakamani kesi iliyofunguliwa na ‘rapa’ kutoka nchini Marekani P Diddy kwa kuishutumu kampuni ya vinywaji ya Diageo kwa ubaguzi wa rangi, hatimaye 'rapa' huyu na kampuni hiyo wamemaliza tofauti zao.

Kwa mujibu wa jarida la ‘People’ Diddy na Diageo wamefikia makubaliano ya kumaliza tofauti zao ambapo ‘rapa’ huyo amefuta mashitaka aliyofungua.

Ikumbukwe kuwa mwezi Mei mwaka 2023 iliripotiwa kuwa Diddy aliishitaki kampuni ya Diageo kwa ubaguzi wa rangi, baada ya kampuni hiyo kutemana naye huku ikidai kuwa vinywaji alivyokuwa akitangaza ‘rapa’ huyo vilikuwa havifanyi vizuri sokoni kwa sababu alikuwa mtu mweusi.

Diddy amefanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka 15, mara ya kwanza alianza mwaka 2007 akiwa anatangaza bidhaa zao, kufikia mwaka jana walitemana na ndipo Diddy akafungua kesi dhidi ya kampuni hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags