Diddy kwenye tuhuma nyingine, unyanyasaji wa kingono

Diddy kwenye tuhuma nyingine, unyanyasaji wa kingono

Mwanamuziki wa hip-hop Diddy kutoka nchini Marekani, kwa mara nyingine tena ameingia kwenye tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.

Awamu hii Diddy ametuhumiwa kumfanyia unyanyasaji wa kingono pampja na kumdhulumu malipo ya uandaaji wa albamu ya ‘The Love Album: Off the Grid’, aliyekuwa Producer wake, Rodney Jones Jr.

Jones amedai kuwa kati ya mwaka 2022 na 2023 akiwa anaishi nyumbani kwa Diddy alilazimishwa ngono na wanawake wanaojiuza, kushiriki mapenzi ya jinsia moja, alishikwa sehemu zake za maumbile na kulazimishwa kutumia Pombe na Dawa za Kulevya.

Hakuishia hapo akaongeza kuwa vitendo hivyo viliambatana na ahadi kutoka kwa Diddy kuwa atampatia tuzo na kufanywa awe maarufu.

Malalamiko hayo yanaenda sambamba na fidia ambayo Jones anataka kulipwa na Diddy. Anasema alipwe Dola za Marekani 30 milioni ambazo ni sawa na Sh76.5 Bilioni. Kwa upande wa Diddy nao hawajakaa kimywa wanasheria wake wamekanusha madai hayo na kudai kuwa siyo ya kweli.Hii itakuwa ni mara ya nne Diddy kutuhumiwa kufanya vitendo vya unyanyasaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags