Diddy haruhusiwi kutaja jina la Cassie hadharani

Diddy haruhusiwi kutaja jina la Cassie hadharani

PBaada ya mkali wa Hip-hop kutoka Marekani kuomba radhi hadharani kufuatia na video ikimuonesha akimshambulia aliyekuwa mpenzi wake Cassie huku mashabiki wakijadiri kuwa kwanini rapa huyo hakutaja jina wakati wa kuomba msamaha ambapo kwa mujibu wa ripoti mpya Diddy haruhusiwi kutaja jina la Cassie hadharani.

Kwa mujibu wa tovuti ya tmz imeeleza kuwa Diddy hajataja jina la Cassie kutokana na wawili hao kuweka makubaliano wakati wa kusuluhisha kesi ya unyanyasaji wa kijinsia iliyofunguliwa na Cassie Novemba 2023.

Katika makubaliano hayo yaliyofanywa na (NDA) yalieleza kuwa hakuna mtu yeyote kati yao anayetakiwa kumjadili mwenzake hadharani kwa namna yoyote ile.

Hata hivyo tmz ilieleza kuwa ili kuepukana na hilo timu ya wanasheria wa Diddy ilipitia msamaha wa video kabla ya kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu walitaka kuhakikisha masharti ya NDA ya kutomtaja Cassie kwa jina.

Ikumbukwe kuwa Diddy aliomba radhi Jumapili Mei 19, 2024 Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kueleza kuwa anaomba radhi kwa kile kilichotokea huku akidai kuwa hakuwa kwenye utimamu wa akili na yuko tayari kwenda kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kuwa mtu mwema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags