Diddy akanusha tuhuma zinazomkabili

Diddy akanusha tuhuma zinazomkabili

Mkali wa hip-hop kutoka Marekani Diddy amekanusha tuhuma zote zilizotolewa na aliyekuwa producer wake Rodney “Lil Rod” Jones akidai kuwa producer huyo alizitoa kwa ajili ya kujipatia pesa.

Diddy kupitia wakili wake Marc Agnifilo, amewasilisha ombi la kufuta malalamiko yaliyotolewa na Jones katika mahakama ya shirikisho ya Manhattan siku ya Jana Jumatatu Agosti 26 na kupinga shutuma hizo huku akieleza kuwa Jones anatumia nafasi hiyo kuchafua jina la ‘rapa’ huyo pamoja na kujiingizia kipato.

Kwa mujibu wa TMZ, Jones hivi karibuni alishiriki video kwenye X akiwa na rapa Uncle Murda ambapo walionekana wakitania kuhusu kesi hiyo dhidi ya Diddy. Katika video hiyo, Jones anadaiwa kusisitiza kwamba Diddy amlipe hizo pesa kufikia Jumatatu.

Hata hivyo mwanasheria wa Diddy ameweka wazi kuwa Jones bado hajathibitisha kuathirika kwa biashara wala mali zake ambazo anataka alipwe na Combs.

Hapo awali, Jones alidai kuwa biashara na mali yake iliathirika kutokana na huduma alizozitoa ambazo hazikulipwa kwa ajili ya albamu ya Diddy ya 2023, iitwayo “The Love Album: Off The Grid.”

Mbali na hilo Rodney Jones Jr amemshitaki Sean “Diddy” Combs katika mahakama ya shirikisho, akimtuhumu nyota huyo wa muziki kujihusisha na shughuli haramu za dawa za kulevya pamoja na unyanyasaji wa kingono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags