Diddy afunguliwa tena mashitaka ya ubakaji

Diddy afunguliwa tena mashitaka ya ubakaji

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani #Diddy amefunguliwa mashitaka mengine ya ubakaji na mwanadada Joi Dickerson-Neal kwa tuhuma za kumpa dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono kwa kumbaka.

Inadaiwa tukio hilo lilitokea Januari 3, 1991, #Joi amedai kuwa baada ya kupewa dawa na kudhalilishwa kingono aligundua kuwa #Diddy ‘alirekodi’ tukio hilo na kuwaonesha marafiki zake.

Hata hivyo mwanasheria wa #Diddy ameeleza kuwa tuhuma hizo za uongo na aliyefungua mashitaka hayo ana nia ya kutaka kujipatia fedha.

Kwa mwaka huu hii si mara ya kwanza kwa #Diddy kufunguliwa mashitaka kama hayo, wiki chache zilizopita mwanamuziki na muigizaji #Cassie alifungua mashitaka dhidi ya #Diddy kwa kumzalilisha kingono pindi walipokuwa kwenye mahusiano zaidi ya miaka 10. Lakini wawili hao walimaliza tofauti zao kwa amani na shauri hilo kufutwa mahakamani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags