Diddy aendelea kuelemewa na mizigo ya kesi

Diddy aendelea kuelemewa na mizigo ya kesi

Baada ya mwanamuziki na dansa kutoka Marekani Cassie, kuweka wazi siku ya Jana Alhamis Mei 23, 2024 kuwa yupo tayari kuwashika mkono wanawake wote ambao wamefanyiwa ukatili, na sasa aliyekuwa mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Mitindo nchini humo aitwaye Lampos amemfungulia kesi Diddy ya kumfanyia unyanyasaji wa kingono.

Kwa mujibu wa Tmz, Lampos alidai kuwa alifanyiwa ukatili na Diddy mwaka 1995 huko Soho katika hotel moja iitwayo ‘Millennium’ ambapo alieleza kuwa Combs alimlewesha siku hiyo na kumpeleka katika chumba cha hotel na kuanza kumlazimisha kufanya naye mapenzi, lakini kwa kuwa alilewa sana alipoteza fahamu baada ya kuamka asubuhi alijikuta yupo mtupu

Aidha aliendelea kwa kudai kuwa miezi kadhaa baadaye Diddy alianza mawasiliano na yeye tena na kumpa nafasi za kufika katika hafla za tasnia ya muziki ndipo Lampos akaamua kumpa nafasi ya pili Diddy akiamini kuwa mara ya kwanza alifanya makosa.

Lakini udhalilishaji huo ulirudia tena siku chache baada ya kusameheana wakati wakielekea kula chakula cha jioni kwenye maegesho ya magari alimlazimisha kufanya naye ngono ya mdomo ingawa kitendo hicho hakikufanikiwa baada ya mhudumu kwenye maegesho hayo kushuhudia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags