Diamond: wenye majengo marefu fanyeni services

Diamond: wenye majengo marefu fanyeni services

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, #DiamondPlatnumz amesema akiwa na msanii, #Jux na watu kadhaa wamenusurifa kifo baada ya ‘lifti’ waliyopanda kuzima huku chanzo kikiwa hakijawekwa wazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram #Diamond ame-post na kushusha ujumbe ukieleza kuwa “Siku ya leo mimi, #Jux, #fole_x na wenzetu kadhaa tumenusurika kifo kwenye ‘lifti’.... Ndugu zangu wenye majengo marefu yenye kutumia ‘lifti’ tujitahidi kuzifanyia #services (ukarabati) hizi ‘lifti’ zetu, ili kuepusha madhara kwa wananchi,"

Bado haijafahamika wasanii hao walikuwa katika jengo gani kwa shughuli ipi huku kukiwa hamna taarifa yoyote ya chanzo cha ‘lifti’ hiyo kuzima ghafla kisha kuwaka na kufunguka ndipo wasanii hao wakatoka  wakiwa na hofu kubwa.

Wasanii hao wakiwa na kundi la watu wengine wametokewa na kisa hicho ikiwa ni mwezi mmoja na wiki mbili tangu tukio lingine la aina hiyo litokee baada ya ‘lifti’ iliyopo katika jengo la ghorofa la #PSPF #MilleniumTower Makumbusho, jijini Dar es Salaam iporomoke na kujeruhi watu watano.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags