Wakati ngoma ya mkali wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz ya ‘Komasava’ ikiendelea kukosha nyoyo za watu kutoka katika mataifa mbalimbali msanii huyo ameweka wazi kuwa wakati anafikiria kufanya ngoma hiyo alikuwa na lengo ngoma hiyo isikilizwe na watu mbalimbali.
Akizungumza katika mahojiano maalumu wakati wa tamasha Afronation linalo endelea nchini Ureno ameweka wazi kuwa wimbo huo aliurekodi Ramadhani ya 27.
“Nilikuwa na producer wangu, nikirekodi na nikasema yoh, ni wakati wa kwenda kuswali Tahajjud, kwa kawaida kama Muislamu unapoomba Mungu akupe chochote unachotaka, nami nikafanya hivyo na baada ya hapo nikarudi studio kurekodi” amesema Diamond
Aidha aliongeza kwa kueeleza kuwa aliamua kutoa ngoma hiyo kwa ajili ya kuwaunganisha watu.
“Wakati tunarekodi wimbo huo tulikuwa tunafikiria kutoa wimbo ambao unaoweza kuwaunganisha watu ndiyo maana nikaweka lugha tofauti, kuna Kifaransa, Kiswahili, Kilatini, Kizulu”
Hata hivyo aligusia kidogo kuhusiana na jina la wimbo huo akidai kuwa ni kutokana na nchi mbalimbali Duniani kote kuongea Kifaransa, rhythm lakini pia pamoja na mapenzi ambayo wanayo nchi zinazoongea lugha ya Kifaransa.
Tangu ilipotolewa Mei 3, 2024, Komasava imepata mafanikio makubwa, ikiwa na zaidi ya watazamaji 3.1 kwenye YouTube, waskilizaji milioni 5.4 kwenye Boomplay, na milioni 1.6 kwenye Spotify.
Leave a Reply