Diamond hakuwa na bajeti ya mashati mwaka 2023

Diamond hakuwa na bajeti ya mashati mwaka 2023

Wasanii wengi wamekuwa wakijitengenezea aina fulani ya kimuonekano ambao mara nyingi huwatofautisha na watu wanaofanya shughuli nyingine, kawaida ukimtazama msanii kama vile Burna Boy na Asake kutoka nchini Nigeria hakika watakushagaza kwa mionekano yao hasa kimavazi.

Ukija kwa msanii kutoka nchini Marekani Kanye West ndiyo kabisa unyama ni mwingi, jamaa kwenye uvaaji aachwe kama alivyo, lakini kibongo bongo nako si kinyonge, wakumuita Simba la Masimba Dangote (Diamond) naye kwenye mitupio ana aina yake ya uvaaji ambayo humfanya awe na muonekano wa kitofauti.

Ambapo utofauti wake huo hupelekea baadhi ya washikaji kumuiga kimitupio, kama ilivyokuwa mwaka 2020 alipoachia wimbo wa ‘Jeje’, huku kwenye kichupa chake (Video) akiwa amepigilia suruali pana (bwanga) na viatu vikubwa, mtaani nako pakaitika mabishioo kibao wakaanza kuvaa nguo pana na viatu vikubwa wakiviita ‘Jeje’.

Sasa imepita miaka mitatu tangu fashion ya ‘Jeje’ kutikisa mitaani, lakini kwa mwaka huu 2023 imekuwa tofauti kwa mkali huyu, unaweza kusema katupilia mbali bajeti ya kununua mashati, kwani katika sehemu nyingi ameonekana akiwa kifua wazi, tena wakati mwingine anapigilia ‘kropu topu’ambayo bado inaonesha maeneo ya kifua chake.

Diamond alionekana miezi mitano iliyopia akiwa kifua wazi kwenye show ya Yanga ('Treble PARADE') iliyofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam, hakuishia hapo bado aliendelea kuonekana kwenye maeneo mengine akiwa katika muonekano huohuo, hata akiwa kwenye safari zake wakati akienda kupanda ndege bado alionekana hivyo huku chini akiwa anabadilisha bukta anazovaa.

Licha ya kuwa kifua wazi Novemba 16 Simba akabadilika kidogo katika siku ya kumtambuisha msanii mpya kwenye 'lebo' ya WCB, ambapo alionekana akiwa amevaa bukta kama kawaida yake huku juu akipigilia shati fupi, ('kropu topu') ambayo haijafungwa vifungo, hivyo ilionesha sehemu ya kifua chake.

Kutokana na muonekano wa msanii huyu kwa mwaka 2023 Noel Gio ambaye ni mbunifu wa mavazi wa msanii huyu wakati akizungumza na Mwananchi Scoop amesema kuwa mwanaume kukaa kifua wazi ni moja kati ya urembo wenye kuvutia, kama ilivyo kwa wanawake kuvaa cheni au hereni kwa ajili ya kujipendezesha, hivyo mwanaume pia hupendeza akiwa kifua wazi, hasa akiwa na mwili mzuri kama ilivyo kwa Diamond na ndiyo maana amekuwa akionekana kifua wazi.

"Nchi yetu imechelewa sana kujua hivi vitu, huko nje ya nchi watu tayari wamekaa sana vifua wazi na kuvaa 'kropu topu', kwa hiyo ndiyo vinakuja sasa Tanzania, vimechelewa sana ni vitu ambavyo kwa wenzetu vilishakuwa 'trendi', 'kropu top' kila mtu anaweza kuvaa bila kuzingatia jinsia lakini ukiwa na muonekano mzuri, mwaka huu unaelekea kuisha, 2024 tunatafuta fashion nyingine". Anasema Noel

Noel anasema licha ya kubuni mavazi ya Diamond huwa anazingati zaidi vazi ambalo msanii mwenyewe ataliridhia na kulipenda. "Mara nyingi nimewahi kumvalisha Diamond na akalikataa vazi, hivyo hata 'kropu topu' kwa kipindi cha nyuma ingekuwa ngumu kumvalisha". Anasema Noel

Hata hivyo wadau wa burudani wamezungumza na mwananchi kuhusiana na muonekano wa msanii huyu kwa mwaka 2023, Peter Minja kutoka Kawe jijini Dar es Salaam anasema msanii ni lazima awe na muonekano utakaoweza kumtofautisha na watu wengine, na ndiyo inaleta maana halisi ya sanaa.

“Msanii ni lazima awe tofauti na watu wengine kimavazi, muonekano na maisha kwa ujumla kwa sababu akiwa kawaida hatakuwa na kitu cha ziada cha kufanya mtu aweze kumfuatilia, ukitazama mtu mpaka unaitwa msanii basi tayari kuna vitu anaweza kuvibadilisha na kuwa kwenye muundo wa sanaa na vikavutia watu wengine.”Anasema Peter

Aidha mdau mwingine wa muziki Caren John kutoka Tabata jijini Dar es Salaam anasema, “Ni sahihi kuwa na muonekano tofauti ili kuweza kutofautishwa, msanii anatakiwa kuwa na muonekano tofauti lakini hakikisha …






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post