Diamond Damu Damu Na Nyimbo Za Kutia Huruma

Diamond Damu Damu Na Nyimbo Za Kutia Huruma

Mwanamuziki Diamond licha ya kufanya vizuri kwa miondoko na midundo mbalimbali ya muziki. Lakini mashairi ya kunung'unika yanaonekana kumbeba zaidi

"Aloiumba leo ni Mungu na ndio ataiumba kesho.
Amini fungu letu laja haliko mbali
Alisema mtazaa kwa uchungu, tutatafuta kwa mateso.
Baby mitihani kawaida usijali, mnh!
Kidogo nnachokuletea usinune pokea
Nipate moyo nifariji"

Hayo ni baadi ya mashairi ya Diamond katika wimbo wa 'Yatapita' ambao mashairi yake yanamuinesha akinung'unika kwa mpenzi wake kisa kipato chake ni kidogo.

Utolewaji wa ngoma za namna hii kwa msanii huyu zinaonekana kuwa kati ya kazi zake ambazo zimekuwa zikipokea mwitikio mkubwa na kufanya vizuri.

Yatapita ni wimbo ambao hadi sasa tangu utoke ni miaka miwili nyuma huku ukiwa umetazamwa zaidi ya mara milioni 60.

Hiyo haikuishi hapo kwa mwanamuziki huyu ambaye ni mmiliki wa lebo ya WCB kwani miaka kumi na moja iliyopita akiwa bado mgeni katika gemu aliachia ngoma yenye mashairi kama hayo nayo ilimleta mjini kwa ukubwa.

"Na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu, Mama
Vyote hukuvijali, hukona silingani kabisa kuwa na wewe
Kwa kuti na mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu mama
Eti kisa maali, ukaona bora uniache mimi na uolewe,"ameimba Diamond wenye Mbagala

Wimbo huo ambao ni kati ya zile zilizofanya akubalike kwa mashabiki hadi sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 18 kwenye mtandao wa YouTube.

Kama haitoshi mwaka 2025 umeanza kwa manung'uniko kutoka kwa msanii huyo ambaye ameuanza kwa kuachia kibao kiitwacho 'Nitafanyaje' chenye mahadhi hayohayo ya kunung'unika kwa mpenzi wake kisa uchumi wake mdogo


"Siwezisema kitandani, labda umasikini wangu
Ndo kinayonishusha thamani waheshiminike wenzangu
Siwezisema skujali (Labda vizawadi vywangu mimi)
Havikufikia ukubwa wanavitoa wenzangu"

Utolewaji wa wimbo huo umefanya video yake itembelewe mara milioni 1.2 kwenye mtandao wa YouTube. Hii inaenda kuipindua ile ngoma yake 'Holiday' iliyotoka Desemba, 2024 ambayo hadi sasa imetazamwa mara milioni 1.4 ndani ya mwezi mzima

Hivyo hivyo imetokea pia kwenye wimbo wake Kamwambie uliotazamwa zaidi ya mara milioni 13, I Miss you (Milioni 31) na nyinginezo

Ikumbukwe kuwa tayari nyota huyu ana nyimbo nyingi zilizofanya vizuri kimataifa ikiwemo Komasava remix Diamond akiwashirikisha Jason Derulo, Khalil Harisson na Chley iliyotoka miezi sita iliyopita ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 13






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags