Diamond: Chege hajawai kushuka kwenye muziki

Diamond: Chege hajawai kushuka kwenye muziki

Mwanamuziki #Diamond usiku wa kuamkia leo akiwa katika tamasha Mtwara amemsifia #ChegeChigunda msanii akidai msanii huyo hajawahi kushuka kwenye muziki tokea anamfahamu na anaendelea kubaki na brand yake kwa miaka mingi.

Hiyo ni baada ya wasanii hao wawili kutumbuiza kwa pamoja katika usiku huo, Diamond akawataka mashabiki wakae mkao wa kula kwani project mpya ya msanii huyo akishirikiana naye itatoka hivi karibuni.

Ikumbukwe Chege ni msanii mkonge akitoke katika kundi la TMK Wanaume Family, na amewahi kuachia ngoma na Diamond miaka saba iliyopia inayofahamika kama “Waache Waoane”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags