Diamond azama dm kwa Jason Derulo, aomba kufanya naye ‘kolabo’

Diamond azama dm kwa Jason Derulo, aomba kufanya naye ‘kolabo’

 Mwanamuziki wa Bongo Diamond amezama upande wa meseji Instagram (DM) kwa mwanamuziki kutoka Marekani Jason Derulo kwa lengo kuomba kufanya naye kazi. 

Diamond kupitia Instastory yake ameshare chati zake na msanii huyo akiomba kufanya naye ngoma ambapo Jason alikubali na kumwambia atume file la wimbo huo kwa ajili ya kuingiza verse yake. 

Wiki hii ni kama wasanii wa Bongo wameamka na kismart kwani naye mwanamuziki Harmonize siku chache zilizopita alishare chati zake na ‘rapa’ Meek Mill akiomba kufanya naye ‘kolabo’. 

Jason Derulo anajulikana kwa nyimbo nyingi Duniani ukiwemo wimbo wa ‘Stupid Love’, pia amefanya ngoma na Wasanii kama Nicki Minaj, French Montana na David Guetta huku kwa upande wa Africa akifanya remix na Msanii Bayanni kutoka Nigeria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags