Diamond aweka wazi sababu ya kuvaa Kimasai kwenye Komasava

Diamond aweka wazi sababu ya kuvaa Kimasai kwenye Komasava

Baada ya kuwepo na minong’ono kupitia mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mashabiki wakihoji kwanini Diamond aliamua kuvaa vazi la Kimasai katika video yake na kwanini asingevaa mavazi mengine kama Kitenge, staa huyo anayeshika namba moja YouTube kupitia ngoma yake ya ‘Komasava Remix’ Diamond amefunguka sababu ya yeye kuvaa vazi hilo.

Kufuatiwa na video inayosambaa mitandaoni ambayo imepostiwa dakika chache zilizopita imemuonesha msanii huyo akitolea ufafanuzi sabababu ya kushoot ngoma hiyo Mkoani Arusha na kuvaa mavazi hayo ni kutokana nan chi nyingi za Afrika kuvaa vazi hilo.

“Tupo Monduli Arusha na kilichotuleta huku ni kushoot nyimbo ya ‘Komasava’ kwenye ile party ya ‘Habari gani’ kwanini tumeamua kushoot huku na kwanini tumeamua kuvaa kimasai ni kwa sababu katika hizi nchi tatu au nchi za Afrika mashariki nyingi zinapendelea kuvaa kimasai na vile vile pia ni nchi zinazoongea Kiswahili kwahiyo tulibidi tuvae vazi linalo wakilisha Kiswahili na vazi hilo ni Kimasai”

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond ‘Simba’ kuvaa vazi la kimasai utakumbuka kuwa mwaka 2021 alitinga na vazi kama hilo katika usiku wa tuzo za BET zilizofanyika Microsoft theatre, Los Angeles, Marekani.

Kichupa hicho kinachoendelea kutamba mjini mpaka kufikia sasa kinazaidi ya watazamaji milioni 4 kupitia mtandao wa YouTube ikiwa na siku nne tuu tangu kuachiwa kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags